Chelsea wako tayari kumruhusu mlinzi wa Uhispania Cesar Azpilicueta kuondoka kwenda Barcelona mara tu watakapopata mbadala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. . (Marca - in Spanish)
Wolves wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke, 31, ambaye anakaribia kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Crystal Palace. (Sun)
Kiungo wa kati wa Chelsea Billy Gilmour anatarajiwa kufanya mazungumzo na meneja Thomas Tuchel kuhusu mustakabali wake, huku Everton wakifikiria kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland mwenye umri wa miaka 21. (Telegraph - subscription required)
Arsenal wanapanga kumtambulisha Oleksandr Zinchenko kama usajili mpya. Inaelezwa ameondoka kwenye kambi ya Manchester City, ili kufanya vipimo na kujiunga na kambi ya Arsenal (Fabrizio Romano).
Manchester City iko tayari kupeleka ofa Brighton kwa ajili ya beki wake wa pembeni Marc Cucurella - mlinzi huyo anakwenda kuwa mbadala wa Zinchenko anayetua Arsenal.
Lingard yuko huru baada ya mkataba wake na Manchester United kumalizika June 30, 2022. West Ham pia inaendelea na mazungumzo ya kumnasa mshambuliaji wa Chelsea Armando Broja. Skysport
Juventus imefikia makubaliano na Torino kuhusu uhamisho wa Gleison Bremer! ada ya €40m imekubaliwa na Torino kwa ajili ya beki huyo wa kati huyo Mbrazil aliyekuwa anasakwa pia na Inter (Fabrizio Romano).
Mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Frenkie de Jong anapinga kujiunga na Manchester United au klabu yoyote ya Uingereza, lakini kiungo huyo wa kati wa Barcelona mwenye umri wa miaka 25 anafikiria kuhamia mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich. (Sport - in Spanish)
Afisa mkuu Mtendaji wa Bayern Munich Oliver Kahn amemtaja mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 28, kama "mshambulizi bora kabisa" na "ndoto ya siku zijazo" baada ya kukubali kumuuza Robert Lewandowski, 33, kwa Barcelona. (Star)
Barcelona wameelekeza nguvu zao kumleta mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Chelsea, baada ya kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa Poland Lewandowski. (Marca)
Bayern Munich wameweka ofa mpya ya £59.5m na £8.5m kama nyongeza kwa beki wa kati wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, huku mazungumzo kati ya klabu hizo yakifikia hatua ya mwisho. (Goal)
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa chini ya dau la euro 2m (£1.7m) kutoka kwa Gent ya Ubelgiji, ambako alikaa msimu huu kwa mkopo, lakini klabu hiyo ya Bundesliga ina thamani yake ya euro 5m (£4.2m (Voetbal Nieuws - in Dutch)
Tottenham wako tayari kulipa euro 17m (£14.4m) kwa mshambuliaji wa Barcelona Memphis Depay, lakini klabu hiyo ya Uhispania inataka euro 20m (£17m), ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 pia anasita kuondoka Nou Camp. Sport - in Spanish)
Bodi ya Barcelona imefanya mazungumzo na Depay kubaini iwapo mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United ana nia ya kubaki au kuondoka. (Fabrizio Romano)