Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Asilimia 45 ya kupoteza muda ni pale unapokuwa umepanga foleni ya kupata huduma kwa mfano Benki, sehemu ya huduma ya maji, hospitali n.k
 
Sababu nyingine zinazopelekea kupotea bure kwa muda ni kama kukaa kwenye foleni za barabarani ambayo utafiti umeonesha ni kwa asilimia 44, matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo utafiti umeonesha yanapoteza muda kwa asilimia 21 na kusubiri kitu kichemke mathalani maji au chai muda hapo hupotea kwa asilimia 15.
 
Matumizi ya mitandao ya kijamiiKatika utafiti huo asilimia 47 ya wazee wamesema wanajikuta wanakaa bila kitu cha kufanya takribani mara tatu kwa siku na hiyo inatokana na kukosa hamasa ya kufanya kazi, na kwa nyongeza tu ni kwamba asimilia 56 ya watu waliohojiwa katika utafiti huo wamekiri kuwa wanatakiwa kulifanyia kazi suala zima la matumizi sahihi ya muda.
 
Katika kupambana na suala la kutunza muda imebainika kuwa asilimia 38 ya binadamu wanapoteza muda wao mwingi katika kuangalia televisheni pamoja na matumizi ya mtandao wa intaneti.
 
Majibu ya watu waliohojiwa kuhusu nini kifanyike ili kuwa na matumizi sahihi ya muda kwa asilimia 70 wamesema watautumia mwaka huu wa 2022 kujifunza njia na ujuzi mbalimbali ili kuokoa muda unaopotea bure.
 
Matukio ya kuuawa kwa viongozi wa juu wa nchi duniani yamekuwa yakipingua kasi katika miongo ya hivi karibuni, lakini hata kwa uchache wake bado yanatokea.
 
Kifo cha Rais wa Haiti Jovenel Moïse aliyeuawa kwa kushambuliwa kwa risasi akiwa kwenye makazi yake, katika mji mkuu, Port-au-Prince ni mfano mmoja tu wa viongozi wakuu wa nchi zaidi ya 100 kuuawa katika kipindi cha miongo 10 iliyopita.
 
Ripoti moja iliyochapishwa mwaka 1998 nchini Marekani ya Military Medicine (Vol. 163), inaonesha kati ya mwaka 1965 mpaka 1996 viongozi wakuu wa nchi 261 walifariki, kati yao viongozi 118 walifariki wakiwa madarakani huku asilimia 44% ya viongozi hao waliuawa. Kati ya Viongozi 144 waliofariki baada ya kutoka madarakani, asilimia 11% waliuawa.
 
Matukio ya kuuawa kwa viongozi hao yanatokea duniani kote, lakini mara nyingi zaidi hutokea katika nchi za masharki ya kati, Asia ya Kusini na nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
 
Ukiacha viongozi wengi huko nyuma kama John Kennedy wa Marekani, Park Chung-hee wa Korea Kusini, Francois Tombalbaye wa Chad, Hafizullah Amin wa Afghanistan, Anwar Sadat wa Misri na Thomas Sankara wa Burkina Faso, BBC inakuletea baadhi tu ya marais hasa kutoka Afrika ambao waliouawa kwa kushambuliwa kwa risasi wakiwa madarakani.
 
Idriss Deby – Chad

Deby ameiongoza Chad kwa miaka 30 mpaka Aprili 2021, alipouawa wakati akiongoza majeshi ya nchi hiyo kukabiliana na waasi waliokuwa wanataka kumuondoa madarakani.
 
Kifo chake kilitokea siku moja tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa 2021, akipata asilimia 80% ya kura zote katika uchaguzi huo wa April 11, 2021.
 
Deby aliingia madarakani kwa mapinduzi na kumfurusha aliyekuwa Rais na mkubwa wake jeshini, Hissene Habre. Hata hivyo uhusiano wao ulianza kuyumba mapema tu baada ya Habre kumtuhumu Deby kutaka kumpindua. Deby akatimkia Libya baadae Iraq alipokusanya nguvu na kurudi nchini Chad mwaka 1989 na kumfurusha Habre.
 
Hata hivyo uasi kwa mika kenda na kenda unaitafuna Chad, ambayo ni moja ya nchi masikini kabisa duniani, ambapo zaidi ya nusu ya watu wake milioni 15.8 wanaishi kwenye umasikini wa kutupwa.
 
Kulikuwa na vikundi vya waasi vilivyoendesha mapigano ya kumuondoa madarakani Deby, ambavyo vilifanikiwa kumchapa risasi walipoukaribia mji wa Djamena na kumjeruhi kabla ya kupoteza maisha.
 
Sheikh Abeid Aman Karume – Zanzibar

Alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar na makamu wa kwanza wa Rais wa Tanzania. Anaheshimika sana visiwani humo kwa jitihada zake za kuileta Zanzibar pamoja, lakini pia kuviunganisha visiwa hivyo na Tanganyika na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…