Sheikh Karume aliuawa kwa kupigwa risasi katika jengo la Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shirazi (ASP) visiwani mjini Zanzibar mnamo tarehe 7 Aprili, 1972.
Anatajwa mmoja wa walinzi wake kufanya shambulio hilo ingawa hakuna uhakika wa hilo mpaka leo, kutokana na kutowekwa wazi kwa taarifa rasmi ya kifo cha kiongozi huyo ambaye hawezi kusahaulika katika historia ya ukombozi wa visiwani humo kutokana na misingi aliyowajengea Wazanzibar.
Anakumbukwa kwa ubabe wake wa vita uliomsaidia kuingia madarakani mwaka 1969. Alikamatwa na kuteswa kiasi kabla ya kuuawa Oktoba 20,2011, kufuatia mapigano yaliyoitwa ‘Battle of Sirte, kati ya wanajeshi wanaomtii na wanajeshi wa NTC wasiomtii kiongozi huyo.
Alikutwa amejificha kwenye kalavati dogo kuwakwepa wanajeshi hao. Zilisambaa video zikiwaonyesha waasi wa NTC wakimpiga kiongozi huyo ambao baadae walimmaliza kwa kumpiga risasi kadhaa. Baade kukaja ripoti ambayo haijathibitishwa kwamba alijiua mweyewe kwa bastola yake. Ripoti inayopingwa na waliokuwa walinzi wake
Waziri mkuu wa NTC , Mahmoud Jibril, ndiye aliyetangaza kifo chake akisema amefariki kwa majeraha ya risasi, ingawa hakusema risasi hizo zimepigwa na nani.
Alikuwa Rais wa tatu wa DR Congo wakati huo inaitwa Zaire. Aliongoza nchi hiyo kuanzia mwaka Mwaka 1997 mpaka alipouawa Januari mwaka 2001. Baada ya kuingia madarakani kwa kumfurusha Mobutu Seseseko, Kabila alibadilisha katiba na kurejesha jina la DRC na kulifuta jina la Zaire
Alipigwa risasi ofisini kwake January16 2001 na kukimbizwa Zimbabwe kwa matibabu. Kifo chake kilitangazwa January 18, ingawa waziri wa afya wa wakati huo, Leonard Mamba aliyekuwa chumba cha pili cha ofisi wakati shambulio likitekelezwa alieleza kwamba Kabila alifariki papo hapo.
Wiki moja baadae mwili wake ulirejeshwa DRC kwa ajili ya mazishi ya kitaifa, kabla ya mtoto wake Joseph Kabila kumrithi na kuwa Rais wa nchi hiyo siku 10 tu tangu baba yake Kabila auawe. Zaidi ya watu 130 walihusishwa na njama za kifo chake akiwemo mmoja wa wapwa zake na kuhukumiwa adhabu mbalimbali.
Vieira aliongoza Guinea-Bissau kwa vipindi vitatu tofauti, alianza mwaka 1980 mpaka1984, akaendelea kipindi cha pili 1984 mpaka 1999, na kipindi cha tatu ilikuwa mwaka 2005 mpaka 2009. Baada ya kuingia madarakani mwaka 1980, Vieira aliiongoza Guinea-Bissau kwa miaka 19 mna akashinda uchaguzi mkuu wa vyama vingi wa mwaka 1994.
Hata hivyo vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1998-1999 vilisitisha utawala wake na kutimkia ng’ambo. Akarejea kwenye siasa mwaka 2005 na kushinda uchaguzi wa rais.
Hata hivyo miaka minne baadae (Machi 2, 2009) akauawa na wanajeshi wake , masaa machache baada ya kuuawa kwa mkuu wa majeshi Jenerali Batsta Tagme Na Waie. Ripoti za kifo chake haziko wazi sana, wapo wanaoamini kauawa kwa bomu na wengine kauawa kwa risasi na baadae bomu.
Hata hivyo Jeshi la nchi hiyo lilikana kuhusika na kuuawa kwake, baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba, Jeshi lililipiza kisasi baada ya baadhi ya wanajeshi kumtuhumu Rais Vieira kuhusika kuuawa kwa Jenerali Waie. Wakati wa utawala wake Vieira aliitambulisha kama zawadi ya Mungu “God’s gift” kwa nchi ya Guinea-Bissau.
Samuel Kanyon Doe, mwanajeshi na nguli la vita, aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki akiwa na wanajeshi wenzake 17 tu na kuwa rais kwa miaka 10 kati ya mwaka 1980 na 1990. Anatambulika kwa utawala wake uliogubikwa na giza kuhusu vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu.
Uchaguzi wa mwaka 1985 alioshinda ulitajwa kuwa wa udanganyifu mkubwa na kuanzia hapo akaanza kuandamwa na wapinzani wake akiwemo Yormie Johnson na Charles Taylor aliyeongoza kundi la National Patriotic Front ili kumuondoa madarakani.
Akiwa njiani kukimbia nchi Septemba 9, 1990 akiwa na walinzi wake karibu 60 lilivamiwa na kundi la Yorme Johnson na akauawa siku iliyofuata. Ukawa mwisho wa Doe aliyetajwa kuwa mmoja wa viongozi madikteta Afrika katika utawala wake wa miaka 10 uliosababisha vifo vya raia wengi wa Liberia
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.