Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ongezeko la taasisi zinazotoa mikopo ‘chap chap’ yenye riba kubwa na kugeuka machungu kwa wakopaji, imeelezwa kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa mdaiwa, kufariki kwa shinikizo la damu au kukimbia kusikojulikana.
 
Mikopo hiyo iliyopachikwa jina la ‘kausha damu’ kutokana na maumivu wanayopata wakopaji wakati wa kurejesha fedha, baadhi ya taasisi zimekuwa zikitoa masharti magumu, ikiwamo kutaifisha mali zikiwemo nyumba, magari na samani za ndani endapo mhusika atashindwa kulipa kwa wakati
 
Uchunguzi uliofanywa na Mwanachi umebaini kuwa wanaoshindwa kurejesha mikopo kwa wakati, wamejikuta mali walizoweka kama dhamana zikitaifishwa na kuuzwa katika mazingira yasiyotoa fursa kuweza kupinga uuzwaji wa mali zao hizo.
 
Taasisi ya mikopo yaelezaMtendaji wa Kampuni ya Jojo Microfinance iliyopo Pugu Bombani, Alice Zebedayo alisema unapotaka kuchukua mkopo huo lazima ununue fomu kwa Sh5,000 kwanza ili usajiliwe kisha hatua zifuate.
 
Akizungumza na Mwananchi, Alice alisema fomu hiyo ikisharudishwa anayekopa anatakiwa atoe Sh5,000 nyingine ili viongozi wa kampuni hiyo wanapokwenda kumtembelea nyumbani kwake waangalie samani za ndani vitakavyowekwa dhamana ya mkopo husika.
 
Kama ukichukua Sh100,000 utapewa Sh90,000 baada ya kukatwa Sh5,000 ya fomu na Sh5,000 ya kukutembelea nyumbani kwako ili kuangalia vitu vitakavyowekwa dhamana; halafu riba ya mkopo ni Sh30,000, hivyo unatakiwa ulipe Sh130,000 kwa mwezi mmoja,” alisema Alice.
 
Akifafanua namna ya kulipa, alisema mtu anapochukua Sh100,000 kila siku anatakiwa kulipa Sh4,300, “na ndani ya mwezi mmoja awe amemaliza na akikosa siku moja kulipa faini ya Sh2000 itamhusu kwa kukiuka.
 
Kwa anayechukua Sh50,000 atalipa Sh65,000 na riba na kila siku anatakiwa atoe rejesho la Sh2,200 na akikosa siku moja anatakiwa alipe faini ya Sh2,000 na inategemea, siku zikiwa nyingi na hela hiyo inazidi kuwa kubwa.”
 
Alisema ukiwa mlipaji mzuri wa marejesho hayo hata kama utahitaji kukopa Sh1 milioni unapewa, lakini riba yake ni asilimia 30. “Tutakubaliana kila siku utoe marejesho shilingi ngapi ndani ya mwezi mmoja, ni makubaliano.”
 

Kanuni ya mkopo ikoje?Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili jijini Dar es Salaam, umebaini kuwepo kwa kasoro nyingi katika baadhi ya wakopeshaji, ujanjaujanja wa kucheza na maneno ya mkataba huku wengi wao wakiweka riba kubwa zinazotakiwa kulipwa ndani ya kipindi kifupi.
 

Kanuni ya mkopo ikoje?Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili jijini Dar es Salaam, umebaini kuwepo kwa kasoro nyingi katika baadhi ya wakopeshaji, ujanjaujanja wa kucheza na maneno ya mkataba huku wengi wao wakiweka riba kubwa zinazotakiwa kulipwa ndani ya kipindi kifupi.
 
Pia, umebaini wapo watu binafsi wanatoza riba hadi asilimia 30 kwenye mikopo hiyo kwa mwezi, vinginevyo mkopaji hupigwa faini kabla ya adhabu nyingine
 
Pia, umebaini wapo watu binafsi wanatoza riba hadi asilimia 30 kwenye mikopo hiyo kwa mwezi, vinginevyo mkopaji hupigwa faini kabla ya adhabu nyingine
 
Kwa mujibu wa kanuni za mkopo midogo ya mwaka 2019 kifungu cha 37, kinamtaka mkopeshaji kutunga sera ya mikopo ikieleza mchakato wa ukopeshaji na nyaraka, masharti ya kukopa, aina ya mikopo na dhamana inayokubalika. Mengine ni pamoja na ukomo wa mkopo kwa kila mkopaji, vipindi vya mkopo na masharti kama riba, ada na changizo na malipo ya mara kwa mara
 
Pia, sera hiyo inatakiwa kuonyesha mchakato wa kuidhinisha mkopo, uwezo wa mkopaji, ufuatiliaji na uthaminishaji na kipindi cha neema kama itawezekana.
 
Pia, sera hiyo inatakiwa kuonyesha mchakato wa kuidhinisha mkopo, uwezo wa mkopaji, ufuatiliaji na uthaminishaji na kipindi cha neema kama itawezekana.
 
Wanachosema wakopaji

Waathirika wakubwa wa mkopo huo ni wanawake ambao wamekuwa wakiishia kufilisiwa mali zikiwemo samani za ndani kama vitanda, majokofu, luninga pamoja na vyombo vya kupikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…