Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dalali huyo alisema hali hiyo imewafanya kwa mwaka kuwa na uwezo wa kuletewa hadi dhamana 50 za wateja ili ziwekwe sokoni huku akieleza wakati mwingine zinashindwa kuuzika kutokana na uthamini wake kuwa tofauti.

“Kuna dhamana nyingine zinakuja zikiwa zimethaminiwa kwa gharama kubwa, lakini mteja akija kuangalia thamani yake haiendani hivyo haziuziki,” alisema Moshi.

Pia, alisema kwa mwaka unaweza kupata hata dhamana za watu 50, huku akieleza kuwa wingi wa madalali umechangia kazi kugawanywa.
 
Dalali huyo alisema hali hiyo imewafanya kwa mwaka kuwa na uwezo wa kuletewa hadi dhamana 50 za wateja ili ziwekwe sokoni huku akieleza wakati mwingine zinashindwa kuuzika kutokana na uthamini wake kuwa tofauti.

“Kuna dhamana nyingine zinakuja zikiwa zimethaminiwa kwa gharama kubwa, lakini mteja akija kuangalia thamani yake haiendani hivyo haziuziki,” alisema Moshi.

Pia, alisema kwa mwaka unaweza kupata hata dhamana za watu 50, huku akieleza kuwa wingi wa madalali umechangia kazi kugawanywa.
 
Scholastica Kevela, ambaye ni Mkurugenzi wa Yono Auction Mart alisema kwa mwaka wanaletewa zaidi ya mali 100 za wateja ambao wameshindwa kulipa madeni yao kutoka taasisi za kifedha na Vyama vya Kuweka Akiba na Kukopa (Saccos).

“Kati ya hizo ndani yake ndiyo kuna nyumba, viwanja, kitu chochote alichoweka dhamana mteja,” alisema Scholastica.

Mkurugenzi wa Cops Auction Marts, Mohammed Mmanga alisema kwa miezi miwili wanaweza kupata hata nyumba 30 ambazo ni dhamana kutoka kwa taasisi za kifedha, ikiwamo benki mbalimbali.
 
Alisema kati ya nyumba hizo wanaweza wakauza au wasiuze hata moja kutokana na wateja kudanganya thamani ya fedha.

“Shida ni kuwa wakopaji wengi huwa hawasomi mikataba kwa sababu wana uhitaji wa hela, wakichukua mikopo wanafanyia kazi tofauti na walichoomba,” alisema Mmanga.

“Riba kubwa zipo kwa baadhi ya taasisi ila sio zote, wakopaji wanapaswa kujua wanakopa ili wafanye nini na wafanye kile walichokusudia, siyo kuchukua mkopo unaenda kumnunulia mke wako Iphone ya Sh3 milioni.”
 
Alipotafutwa Katibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Twaha Mwakioja alisema kwa mujibu wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 na Kanuni Zake za Mwaka 2019, biashara ya huduma ndogo za Fedha inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wameweka ukomo wa riba, kiwango ambacho hakizidi asilimia 3.5 kwa mwezi.

“Kwa mujibu wa kanuni ya huduma ndogo za Fedha (majukumu ya waziri) ya mwaka 2019, wizara imeteua waratibu 212 kila mkoa na halmashauri, hivyo tunaomba nyaraka za mkopaji ikiwa ni mkataba wa mkopo ili tuweze kufuatilia na kuchukua hatua,” alisema Mwakioja.
 
Kauli ya BoT

Kwa mujibu wa taarifa ya BoT, wananchi wametakiwa kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni, mtu na watu binafsi ambao hawana leseni.

Hiyo ni baada ya kubaini kuna taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na leseni husika hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha,” inaeleza taarifa ya BoT.
 
Kwa mujibu wa Kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua Sh20 milioni au kifungo kwa muda usiopungua miaka miwili.

“Orodha ya taasisi, kampuni na watu binafsi wenye leseni za biashara ya kukopesha zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ambayo ni www.bot.go.tz
 
Wrap rage' ni hali ya hasira kali na kuchanganyikiwa kidogo inayotokea pale unaposhindwa kufungua kitu fulani!
 
Back
Top Bottom