Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tafiti: Uume uliosimama wastani una urefu wa 13.12 cm, wakati mzingo (mduara) ni 9.31 cm.
 
Tafiti: Tunapendelea kutoka kimapenzi na watu ambao wanavutia (uzuri, kitabia..) karibia wastani wa 25% kuliko sisi!

Hii ni kwa wote, Wanaume na Wanawake!
 
Tafiti: Wanandoa kwa wastani kwa wiki hufanya tendo la ndoa mara moja!
 
Pombe huwa inavuruga uwezo wa kutofautisha sura za watu vizuri, na hiyo ndio sababu mojawapo kila sura huonekana kuvutia ukiwa umelewa!
 
Abebe Bikila kutokea Ethiopia ndie alikua MuAfrica wa kwanza kushinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka 1960, Rome.

Aliibuka mshindi huku akiwa anakimbia bila kuvaa viatu!
 
Phagomania' ni hali ya kisaikolojia inayomfanya mtu kupenda chakula kuliko kawaida!

Mtu mwenye changamoto hiyo akiona chakula tu akili yote itahamia hapo mpaka ale ndio mambo mengine yanaweza kuendelea!
 
Tafiti: Baada ya kushiriki tendo la ndoa unapitia "Transient Global Amnesia"

Ni hali inayokufanya kupoteza kumbukumbu kwa saa kadhaa!

Note: Wote kwa pamoja mfurahie tendo la ndoa!
 
Tafiti: Wanawake wafupi huwa wana bahati ya kudumu kwenye uhusiano na Wanaume kwa muda mrefu zaidi tofauti na Wanawake warefu!
 
Tafiti: Wanawake wenye urefu kuanzia 5ft kushuka chini huwa wana wivu zaidi tofauti na wale wenye urefu kuanzia 5ft kwenda juu
 
China ina zaidi ya wavutaji wa sigara milioni 350, idadi ambayo ni kubwa kuliko hata idadi ya watu pekee ya nchi ya Marekani!

China ndio watumiaji pia wazalishaji wakuu wa tobacco Duniani!
 
Kupeleka Wanasayansi kwenye Kituo cha Kimataifa cha anga aa juu (ISS) na kukaa huko kwa siku 08 tu, wastani wa gharama nzima itayotumika ni $55M (Tzs. Bilioni 128.2).
 
Tafiti: Watu wanaotumia muda mwingi kushinda mtandaoni wana uwezekano mkubwa wa kusumbuliwa na Sonona (Depression), Upweke na matatizo mengine ya akili kwa mujibu wa Utafiti.
 
Climacophilia' ni moja ya aina ya Paraphilia' ambayo mtu anajisikia raha mfanano sawa na mtu anaefanya mapenzi pale anapokuwa anashuka/akianguka kwenye ngazi!
 
Back
Top Bottom