Mtoto alimuomba mama yake amuelezee uzoefu wake katika maisha na hekima alizozozichukua kutoka katika maisha, akamuuliza:
je waweza kusikiliza? akamjibu: ndiyo... basi mama akamwambia:
mwanangu:
Ole wako na minon'gono, usiamini kila lisemwalo wala nusu ya unayoyaona, na kama Mola akikupa mtihani wa adui, pambana naye kwa wema, kwani wema una nguvu kuliko uadui.. peleka lililo bora
Ukitaka kumjua rafiki safiri naye, kwani katika safari binadamu anajulikana uhalisia wake na muonekano wa nje unafifia na ukweli wake hujulikana, na ndiyo maana ikaitwa safari kwa sababu tabia hujitokeza
Watu wakikuhujumu huku ukiwa kwenye haki furahi!
kwani wanakwambia wewe ni mwenye mafanikio na mwenye taathira na haulengwi mawe ila mti wenye matunda
Mwanangu.. pindi ukimkosoa mtu yoyote
jizoeshe kumuangalia kwa jicho la nyuki
usimuangalie kwa jicho la nzi ukaangukia kwenye uchafu
Lala mapema mwanangu kwani baraka ya riziki iko asubuhi, na nakuogopea usije ukaikosa riziki ya Mola kwa sababu ya kukesha
Na nitakusimulia kisa cha kondoo na mbwa mwitu ili usije ukamuamini anayekufanyia kinyume
Kama kuna mtu anakuamini, ole wako kisha ole wako kumfanyia khiana
Nitakueleza kuhusu simba na nitakufundisha kwamba simba hajakuwa mfalme kwa sababu ya kubweka, lakini ni kwa sababu ana nafsi azizi,
hachukui windo la mwenzake hata akiwa na njaa gani.. kwa hiyo usiibe juhudi ya mwenzako ukafanya jeuri!
Nitakwenda nawe kwa kinyonga ili ushuhudie mwenyewe hila yake! yeye huifanya ngozi yake ifanane na rangi ya sehemu, basi tambua kwamba watu ni kama kinyonga, kopi zinazojirudia
Jizoeshe ewe mwanangu kushukuru
mshukuru Mwenyezi Mungu, ikutoshe kwamba wewe unakwenda unasikia unaona.. mshukuru Mwenyezi Mungu na washukuru watu kwani Mwenyezi Mungu anawazidishia wanaoshukuru
na watu wanampenda mtu ambaye ukimfanyia jambo anathamini
Fadhila kubwa katika maisha ni ukweli na tambua kwamba uongo japo unaweza kuokoa lakini ni katika ubaya mkubwa
Mwanangu.. Jiwekee mbadala wa kila kitu, jiandae kwa jambo lolote ili usije ukaomba na kudhalilika,
na faidika na kila fursa kwani fursa inayokuja sasa haijirudii
usilalamike wala usibabaike!
nataka uwe mwenye matumaini ukiyakabili maisha, wakimbie wakata tamaa na wavunjika moyo, na ole wako kukaa na mtu anayejikweza!
Usifurahie msiba wa mwenzako, na ole wako kukejeli umbo la mtu, kwani mtu hajajiumba
Isomeni kwani ni katika makala nzuri niliyowahi kuisoma