myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
👍Baada ya mazungumzo, mara Massata ananifahamisha kuwa kocha wake kwa jina Lamine ndiye mwokozi wake. Bila Lamine hali yake ingekuwa mbaya mno. "Nazungumzia umuhimu wa kuwa na mahusiano mema." Massata ananifahamisha kisha anamuita kocha wake.
Sawa kabisaTangu agundue umuhimu wa kufanya mazoezi, Massata, hajawahi kuwa mvivu katika maisha mapya aliyoanza kuyaishi. "Hapa huwa ninakuja kufanya mazoezi kuanzia siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, isipokuwa mwishoni mwa juma. Misuli inahitaji kupumzika ili ikue." Massata ananifahamisha huku akiwa kwenye eneo ambalo hufanyia mazoezi akiwa na nguo za mazoezi.
✔️✔️Kabla nianze kufanya mazoezi, nilikuwa na uzani wa kilo 86, lakini sasa uzani wangu ni kilo 76. Mazoezi yalinasaidia kupoteza kilo 10 kwa kipindi cha miezi mitatu." Massata anasema huku akionekana akiridhishwa na hali yake sasa.
Anaafiki kuwa mazoezi yana nafasi kubwa sana maishani mwake sasa. Zamani hakuwa na muda alioutenga kwa ajili ya mazoezi lakini sasa anasema, "mimi hufanya mazoezi kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
👍👍👍Ugonjwa aliokuwa akiugua ni kuwa ini huzungukwa na mafuta. Mara nyingi watu wenye ugonjwa huo, huwa hawaoneshi dalili zozote.
Hadi kufikia sasa hakuna dawa au matibabu ambayo yamethibitishwa kuponya ugonjwa wenyewe. Hata hivyo mabadiliko ya tabia ya kula pamoja na mazoezi ya mara kwa mara ni dawa mjaarabu kwa mujibu wa matabibu.
👍✔️Aliamua kuanza kuyafanya mazoezi kila siku, baada ya miezi mitatu alirudi kufanyiwa uchunguzi tena. "Uchunguzi wa daktari uligundua kuwa maini yangu yalikuwa yanaanza kurejea kawaida." Massata ananifahamisha huku akitabasamu
Bila ya matatizo..Anakiri kuwa mazoezi yalimsaidia kupunguza uzito. Mara ya pili aliporudi kuchunguzwa na daktari wake, alifahamishwa kuwa ini lake lilikuwa sawa kabisa bila ya matatizo.
✔️✔️✔️Misongamano ya magari, kazi za ofisini, kutazama televisheni, kurambaza kwenye mitandao ya intaneti ni baadhi ya mambo ambayo huwafanya watu kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu.
AiseeDaktari alimfahamisha kufanyiwa uchunguzi kwenye figo zake. Kwa bahati nzuri, matokeo ya uchunguzi yalibainisha kuwa hakuwa na tatizo lolote kwenye figo zake. Kwa bahati mbaya uchunguzi uligundua kuwa alikuwa na mafuta kwenye maini yake.
✔️👍👍Inakadiriwa kuwa unapokaa kwa zaidi ya saa nane kwa siku, unastahili kufanya mazoezi ya dakika 60 -75 kila siku, ili kufidia muda uliokuwa umeketi.
📌📌Daktari Mounir Dia wa Senegal anasema kuwa: "Kuna viungo vingi vya mwilini ambavyo huathiriwa kwa kukosa kufanya mazoezi." Anaongeza kusema kuwa, "mtu asipoyafanya mazoezi, kuna uwezekano mkubwa wa mapigo ya moyo wake kuongezeka na ni rahisi kupata magonjwa ya moyo."