Manchester United wanamyatia beki wa Everton mwenye umri wa miaka 21 Jarrad Branthwaite, ambaye thamani yake ni kati ya pauni milioni 60-70. (Sky Sports)
Manchester United inazingatia mkataba wa kubadilishana unaohusisha mshambuliaji wa Uingereza Mason Greenwood, 22, na mshambuliaji wa Ureno na Atletico Madrid Joao Felix, 24. (Star)
Everton na West Ham wameanza mazungumzo na Burnley kuhusu mpango wa kumnunua beki Mfaransa mwenye umri wa miaka 22 Maxime Esteve. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Real Madrid wanapanga kutangaza usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa na Paris Saint-Germain Kylian Mbappe, 25, kabla ya michuano ya Euro msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano
Chelsea italazimika kuchangisha pesa kupitia mauzo ya wachezaji kabla ya Juni 30 ili kuzingatia kanuni za faida na uendelevu za Ligi Kuu ya England. (Sun)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta yuko kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu kandarasi mpya ambayo itamfanya awe mmoja wa makocha wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu. (Mail)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.