Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ripoti ya hivi karibuni ya Hali ya Hewa huko Ulaya, iliyochapishwa Aprili 2024 na European Union's Copernicus Climate Service, ilifichua mabadiliko katika bahari; rangi ya kijani iko kwa 200-500% kuliko kawaida katika bahari ya Norway na Bahari ya Altantic kaskazini mwa Uingereza mwezi Aprili 2023.
 
Lakini rangi hiyo ilikuwa chini kwa 60-80% katika bahari ya magharibi ya Peninsula ya Iberia. Bahari ya Mediterania kiwango cha rangi ya kijani ni 50-100% juu kuliko ilivyokuwa awali. Vipimo hivyo vilichukuliwa kuanzia 1998-2020
 
Uchambuzi wa BBC News wa halijoto ya bahari iliokusanywa na taasisi ya Copernicus - umefichua kuwa bahari duniani zinakabiliwa na ongezeko la joto. Ilionyesha kuwa joto baharini lilizidi kila siku katika mwaka uliopita.
 
Miongo miwili ya kutumia satelaiti za Nasa pamoja na wanasayansi kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT), waligundua kuwa zaidi ya nusu ya eneo la bahari duniani - 56% - limebadilika rangi. Eneo hili ni kubwa kuliko ardhi yote ya dunia.
 
Tunaona mabadiliko katika mabonde yote makubwa ya bahari - kwenye Pasifiki, Atlantiki na [bahari] za Hindi. Haya ni mabadiliko makubwa ya kimataifa ambayo tunaona," anasema B B Cael, mwanasayansi kutoka National Oceanography Centre huko Southampton, Uingereza.
 
Mwaka 2019, Dutkiewicz alitumia kompyuta kutabiri mabadiliko ya baadaye katika rangi ya bahari. Hata hivyo, ilikuwa vigumu kubainisha ikiwa hilo lilitokana na mabadiliko ya hali ya hewa au mifumo ya kawaida ya bahari.
 
Vipimo vya satelaiti vinaendana na kile kinachoonekana kwenye taarifa yake," anasema. "Kwa hivyo, mabadiliko tunayoyaona katika ulimwengu yana uwezekano ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na binadamu."
 
Hii itasababisha mabadiliko kwa viumbe vidogo vya baharini wanaokula phytoplankton, huku utajiri wa spishi ukitarajiwa kupungua na kuongezeka kwa joto la bahari, na kusababisha athari zaidi katika chakula na samaki wanaotegemea viumbe hawa.
 
Back
Top Bottom