Vitu vingi kwenye dunia kwasasa havipo sawa, Watu wengi kwenye dunia kwasasa hawapo sawa, unayemwona hana tatizo leo wala sio ajabu kusikia kesho amejiua, tunaishi kwenye dunia ambayo watu wana vita nyingi rohoni mwao, ukipata wasaa wa kumnenea Mtu mema usiache, ukipata wasaa wa kumwambia Mtu unampenda fanya hivyo, watu wanahitaji sana faraja kutoka kwetu.