Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kuwa Dukani Mara kwa Mara kwa Uaminifu Zaidi. Kama hauna mteja wa kumpelekea mzigo, hakikisha uko dukani kwa mshirika wako. Hii itakusaidia kupiga picha nyingi ukiwa dukani unahudumia watu, na hivyo kuongeza uaminifu wako kwa wateja wako. Pia, itakusaidia kuhakikisha kwamba bidhaa zako zinauzwa kwa bei sahihi hata kama haupo. Ikiwa mteja aliyenunua kwako kwa bei fulani atakuja dukani na kuuziwa kwa bei ya chini, anaweza kuona kama umemdanganya na hatarudi tena