Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Fisi ni myama aishiye mbugani, ambaye anasifa kemu kemu kwa wanadamu, pengine hii nikutokana na kutokeza katika simulizi nyingitulizokuwa tukijifunza katika hadithi, pinditulipokuwa shule ya msingi, ana umaarufu wajina la bwana afya wa porini, hii ni kutokana nasifa yake ya kula mizoga,
 
Mnyama huyu ni maarufu na pengine ndiyemnyama pekee mwenye kufahamika zaidikatika bara la Afrika, hususani hapa nyumbani,kwani mbali na kutokea katika hadithi, lakini piamnyama huyu baadhi ya makabila humtumiawanapocheza ngoma za asili, pia ana sifa yakuhusishwa sana na imani za kishirikina,baadhi ya jamii anapoonekana hupigwa mpakakufa kwa imani kwamba ni mtu amejibadilishakuwa fisi.
 
Jamaa hawa yaani fisi huishi kifamilia na kwataarifa yako ni kwamba hujenga kabisa sehemu wanazokaa, urefu wao ni zaidi ya nchi 35, huwana uzito wa kilo zaidi ya 75 inategemea naumri, huishi zaidi ya miaka 20, hubeba mimba kwa miezi mitatu na akizidisha ni siku chache sana
 
huzaa watoto kuanzia wawili mpaka wanne, kichwa chake hufanana na mbwa ilatofauti yao ipo katika muonekano, fisi ni mnyama ambaye miguu yake ya nyuma ni mifupi zaidi, hivyo unaweza ukamgundua kwa jinsi anavyotembea na matendo yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…