Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pamoja na kwamba ni mnyama ambaye jina lake linakuzwa sana kwamba anatabia ya kula mizoga, lakini fisi ni mnyama anayewinda na hula nyama fresh, akikosa mawindo yake hufanya uporaji kwa wanyama kama simba na inapokosekana hata nafasi hiyo, basi akikutanana mfupa,mzoga yeye hana neno.
 
huzaa watoto kuanzia wawili mpakawanne, kichwa chake hufanana na mbwa ilatofauti yao ipo katika muonekano, fisi nimnyama ambaye miguu yake ya nyuma nimifupi zaidi, hivyo unaweza ukamgundua kwajinsi anavyotembea na matendo yake
 
Wakati wanyama wengine wengi wakiwa wanaongozwa na madume, ukifika katika kooza fisi majike ndio viongozi, lakini mbali na uongozi pia fisi jike ana nguvu za mwili kulikodume, bahati waliyonayo mbaya wanyama hawa hupata tabu sana ya uzazi pindi jike lijifunguapo, watoto wao wengi hufa wakati mama yao anapozaa, hivyo kama jike atazaa wakati dume halipo ana nafasi kubwa ya kuzaa watoto wafu, kwani fisi dume hutoa msaada kwa jike wakati wa kuzaa hasa ulinzi.
 
Fisi ni mnyama anayeweza kukimbia umbali mrefu kwa taratibu, we tangulia na spidi 120 yeye atakuja na 30 na atakukuta tuu njiani ukiwa umeanguka either kwa kuishiwa nguvu au misuli kukaza na hapo ndio atafanya biashara yake kwa urahisi, na sifa hii ndio watu husema eti anasubiri mtu adondoshe mkono wala sio kweli, ana akili zake.
 
Fisi hunguruma, hucheka pia hutoa milio mbalimbali inategemea na alipo, na hiyo huwa nilugha wanayotumia kuwasiliana akifanya hivyo wenzie wakisikia wanajua tuu kuna jambo gani limemsibu mwenzao.
 
Fisi jike huwa na muonekano wa jinsia mbili,katika uke wake kwa juu au sehemu ambayo mwanamke hukeketwa, ile sehemu kwa fisi huwa na ukubwa mkubwa sana inaweza fikanchi saba, jambo hilo humfanya aonekane na muonekano wa jinsia mbili.
 
Fisi wakikosana kwa kuibiana chakula audume, na kwa bahati mbaya mmoja aweMdogo, hupigana mpaka Mdogo kufa, na kamawapo sawa mnyonge hukimbia, wakati huodume hubaki likishangaa tuu na kushindwalianzie wapi.
 
Fisi wakikosana kwa kuibiana chakula au dume, na kwa bahati mbaya mmoja awe Mdogo, hupigana mpaka Mdogo kufa, na kama wapo sawa mnyonge hukimbia, wakati huo dume hubaki likishangaa tuu na kushindwa lianzie wapi.
 
Back
Top Bottom