myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Maisha yana mitihani ila Maisha yenyewe sio mtihani,hivyo hakuna anayefeli au kufaulu maisha,maisha ni uwanja wa mafunzo na elimu haina mwisho, walio pita walijifunza, tuliopo tunajifuna na wajao watajifunza,hakuna kufeli wala kufaulu bali kuna kuishi na kujifunza to enjoy vyote
Kweli kabisa hiliNingumu kupata stori ya mafanikio isiyo na mchango wa bahati ndani yake
Ushindi si wa wenye nguvu zaidi, bali wa wale wasiokata tamaa. Kila siku unapoamka na kuendelea kupigania ndoto zako, unakuwa mshindi tayari.
Asubuhi ya chai
Mwanga hauhitaji kuwa mkali ili kuangaza giza. Hata mwanga mdogo wa tumaini unaweza kuleta mabadiliko makubwa. Endelea kung'aa, haijalishi hali ilivyo.
SawasawaShuleni wana kufundisha somo na kisha kukujaribu kwa mitihani, lakini maisha yana kujaribu kisha yana kufundisha.
💯💯Maisha ni leo sio jana wala kesho, Unachokipitia leo ndio tafsiri sahihi ya Maisha. Mambo ya jana na kesho Achana nayo, Maisha ni Leo.
Nakubaliana na hiliUjasiri sio kutokuwepo kwa hofu, bali ni uwezo wa kusonga mbele licha ya hofu. Kila giza lina mwisho wake, na kila maumivu huzaa nguvu mpya
Umakini muhimuKuwa makini sana, Urafiki na Unafiki vimetofautiana Herufi Moja Tu.
Maisha ni leo sio jana wala kesho, Unachokipitia leo ndio tafsiri sahihi ya Maisha. Mambo ya jana na kesho Achana nayo, Maisha ni Leo.
Ujasiri sio kutokuwepo kwa hofu, bali ni uwezo wa kusonga mbele licha ya hofu. Kila giza lina mwisho wake, na kila maumivu huzaa nguvu mpya