Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Moja ya sumu inayotafuna taratibu ni sumu ya kujilinganisha na wengine, itatafuna furaha yako, mahusiano yako, confidence yako....itakubadili mpaka jina utaanza kujiita mim sii lolote
 
Soma zaidi yao, jifunze zaidi yao, tafuta maujanja ya tofauti, kua mtu mwenye cha ziada, mtu mwenye nyongeza, dunia nayo itakupa zaidi, utapata nafasi ya tofauti, utapewa ziada. kataa kua wa kawaida
 
Nina uhakika hakuna mtanzania anayependa umasikini, kila mmoja anapenda maisha mazuri" - Rais Magufuli
 
Nirahisi kujifunza tabia mbaya kuliko kujifunza tabia njema, uvivu unavutia kuliko uchapa kazi.....kaa mbali na waouvu, tunda lilo oza linaweza kuambukiza wadudu tunda zima,ila zima haliwezi ambukiza uzima kwa tunda bovu
 
Kujielimisha ni kutafuta ukweli wa mambo.”-Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
 
Kuwa mtu mwema, kusema ukweli, kusamehe, kutubu hizi ni fursa ambazo unabarikiwa nazo kila unapofungua macho yako kuiona siku mpya. Chaguo ni lako kuzikamata au kuziacha ziende zake
 
Mwenye ufahamu nusu ni hatari kuliko asiye na ufahamu, kwakuwa yeye huwa aminisha watu kuwa ana fahamu, na huishia kuwa poteza
 
Unapoona umepata tatizo kwenye maisha yako, mkimbilie Mungu kwanza kabla ya watu wengine.” - Charles Stanley
 
Hata hivyo maishani, mambo huwa hayaendi jinsi tunavyotarajia au tunavyotaka.Lakini ni muhimu kuwa na mtazamo chanya maishani na wala sio hasi, na hiyo ndio sababu ninajitahidi kuishi bila kujuta wala sina kinyongo."
Mesut Ozil
 
Usitegemee kuishi maisha chanya kama unaambatana na watu wenye mtazamo hasi.” - Joel Osteen
 
Njia nyingine ya kuacha kuwaza mambo kupita kiasi ni kuyaweka katika mtazamo" Timothy Presley
 
Mtunzaji Pekee Wa Furaha Yako Ni Wewe Mwenyewe.
Acha Kuwapa Watu Nguvu Ya Kudhibiti Tabasam Lako, thamani Yako Na Mtazamo Wako.
 
Yule ambaye hajiamini kufanya jambo lenye hatari, hataweza kushinda chochote katika maisha yake.”-Mohammed Ali
 
1759308421058.jpg
 
Elimu nusu, maarifa nusu, taarifa nusu, imani nusu,dhamira nusu na jitihada nusu haviwezi kukupa matokeo kamili. Utavuna kadri unavyowekeza!" ~Togolani Mavura.
 
Kama kuna kitu hukipendi maishani mwako, kibadilishe. Kama huwezi kukibadilisha basi badili mtazamo wako" ~ Maya Angelou
 
Back
Top Bottom