Moja ya sumu inayotafuna taratibu ni sumu ya kujilinganisha na wengine, itatafuna furaha yako, mahusiano yako, confidence yako....itakubadili mpaka jina utaanza kujiita mim sii lolote
Soma zaidi yao, jifunze zaidi yao, tafuta maujanja ya tofauti, kua mtu mwenye cha ziada, mtu mwenye nyongeza, dunia nayo itakupa zaidi, utapata nafasi ya tofauti, utapewa ziada. kataa kua wa kawaida
Nirahisi kujifunza tabia mbaya kuliko kujifunza tabia njema, uvivu unavutia kuliko uchapa kazi.....kaa mbali na waouvu, tunda lilo oza linaweza kuambukiza wadudu tunda zima,ila zima haliwezi ambukiza uzima kwa tunda bovu
Kuwa mtu mwema, kusema ukweli, kusamehe, kutubu hizi ni fursa ambazo unabarikiwa nazo kila unapofungua macho yako kuiona siku mpya. Chaguo ni lako kuzikamata au kuziacha ziende zake
Hata hivyo maishani, mambo huwa hayaendi jinsi tunavyotarajia au tunavyotaka.Lakini ni muhimu kuwa na mtazamo chanya maishani na wala sio hasi, na hiyo ndio sababu ninajitahidi kuishi bila kujuta wala sina kinyongo."
Mesut Ozil