Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kukata tamaa sio tu kuacha kufanya jambo au kufeli, kukata tamaa pia kuna maana kukubali nafasi ulipo wakati ndani yako unajua kabisa hapa sipo napaswa kua na unajua kabisa kwamba ukipambana zaidi utakua mbali zaidi ya hapo lakini umekubali tu kua hapo, huko nako nikukata tamaa
 
Mthamini na mshukuru yule aliyekunyooshea mkono na kukupa sapoti
 
Fanya siku ya mtu iwe ya furaha, itakufanya wewe pia kuwa na furaha.
 
Kama hukipendi kitu kibadilishe. Kama huwezi kukibadilisha, badilisha mtazamo wako."- Maya Angelou
 
Shauku pekee inayoniongoza ni ukweli ... Huwa naangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo huu".

~Che Guevara
 
Amani ya MOYO nizawadi adim sana linda furaha yako kwa kutoruhusu kelele za dunia kuizima
 
ukijipata kisawa sawa katika kuishi maisha yenye maono utaelewa kuwa hakuna maana nyingine ya maisha zaidi ya kutamani DUNIA ikukumbuke kwa mambo gani uliyo SULUISHA ama uliyo SABABISHA.
 
Maisha ni Fumbo ambalo kila mtu anatafuta namba yakulifumbua kwa namna yake
 
Hakuna shamba linalofanana na maisha ya binadamu wala hakuna kundi la mifugo linalofanana na maisha ya binadamu"
 
Kuwa na tabia ya kuandika malengo yako, alafu yapitie kila wakati na uyafanyie kazi.
 
Onyesha mtazamo na msimamo wako, lakini uwe na uvumilivu na kuheshimu ya wengine.
 
Kamwe usijute kwa kitu chochote, jifunze kutokana na kila kitu.
 
Nyoka hubadili ngozi lakini sum hubaki ileile, vivyo hivyo baadhi ya watu hujifanya kubadilika lakini tabia zao hubaki pale pale. Kua makini usikubali kuumizwa mara mbili
 
Back
Top Bottom