MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU.
Hapa ndipo pana miujiza ya Mungu, kwani
huwezi kufikiria kirahisi kwamba ni kiasi gani
damu ya TWIGA inaweza kusafirishwa kutoka
kwenye moyo hadi kwenye ubongo kutokana
umbali uliopo kati ya viungo hivyo
vinavyotenganishwa na shingo ndefu.
Lakini Twiga kawekewa mazingira ya aina yake
ya kuhakikisha mfumo wa damu unafanyika
bila tatizo lolote licha ya kuwa na maumbile
tofauati na wanyama wengine ya kuwa na
shingo ndefu inayotenganisha kichwa na moyo
Kwa haraka haraka ukimwangalia Twiga
unaweza kuona kuwa maumbile yake
yangeweza kuwa shida katika mfumo wa
kusafirisha damu kutokana na tofauti ya
umbali kati ya kichwa na moyo,lakini mungu
amemuumba Twiga katika
mazingira yanayomuwezesha jambo hili
kufanyika bila shida.
Kwanza moyo wa Twiga unakadiriwa kuwa na
uzito wa kilo 10 na urefu wa sentimeta 60,
hivyo una uwezo wa kuzalisha mgandamizo wa
damu mara mbili ukilinganisha na wanyama
wengine.
Hali hii husaidia kuupa nguvu mfumo wa
kusukuma damu kwenda kwenye ubongo ulio
kwenye kichwa kwa kuwa huwa kipo mbali
kutokana na shingo ya mnyama huyo kuwa
ndefu sana.
Pia karibu na shingo ya mnyama huyo pia kuna
mfumo tata ulioumbwa kwa ajili ya kuminya
damu hiyo kwenda kwa wingi kwenye ubongo
pindi mnyama huyo anapoinamisha shingo.
MAAJABU YA USINGIZI WA TWIGA.
Twiga ni miongoni mwa mamalia wanaolala
muda mfupi zaidi kuliko wote ambapo hutumia
wastani wa dakika 10 hadi saa mbili katika saa
24 za siku.