Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mawimbi kwenye mfumo wa fahamu husafiri kwa kasi ya mita 120 kwa saa (kilometa 200 kwa saa)
 
Inaelezwa kuwa unapomgusa mtu au kitu kinapomgusa mtu, tarifa za tendo hilo husafiri kwa kasi kubwa ya mita 120 kwa saa (kilometa 200 kwa saa) kuelekea kwenye ubongo.
 
Waatalamu wa afya wanaeleza kuwa binadamu huvuta hewa takriban mara 23,000 kwa siku moja.
 
Inaelezwa kuwa mwili wako una kaboni nyingi kiasi cha kutosha kuzalisha penseli 900 ikiwa kaboni hiyo itakusanywa.
 
Kwa kipindi cha maisha ya binadamu yote, ubongo wake unaweza kutunza biti za data zipatazo milioni bilioni moja. Milioni bilioni moja? Ndiyo, milioni bilioni moja na zaidi.
 
Nini? Ndiyo, moyo unaweza kuendelea kudunda hata ukiwa nje ya mwili ikiwa tu utapata oksijeni.
 
Moyo umeumbwa kwa namna ambayo unazalisha mawimbi yake ya umeme wenyewe yanayowezesha misuli yake kusukuma damu. Hii ndiyo sababu wataalamu wa tiba wanaweza kuutoa moyo na kuurudisha tena bila shida.
 
Ikiwa mtu atakikosa kidole cha mwisho au kidogo cha mkono wake, basi nguvu za mkono wake zitapungua kwa asilimia 50.
 
“Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili maono yao kuwa uhalisia”
 
Wakati kwenye maeneo mengine kubusu au kukumbatiana kati ya mwanamke na mwanaume ni jambo la kawaida, kwenye maeneo mengine ni kosa kubwa.
 
Baadhi ya nchi za kimagharibi zimewapa raia wake uhuru kiasi cha kuweza hata kufanya matendo ya faragha hadharani.
 
Lakini baadhi ya nchi, hasa zile zenye misingi imara ya kidini, zimepiga marufuku kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…