Qatar ni nchi yenye utamaduni wa Kiislamu ambayo hairuhusu mtu kubusu au kukumbatiana hadharani. Hata hivyo matendo haya baina ya wanafamilia au marafiki wa jinsia moja (wasio mashoga) siyo jambo baya.
India Kwa mujibu wa sheria za India, mtu atakayekutwa akifanya au kuonyesha maswala ya kimapenzi hadharani anaweza kukabiliwa na kifungo kisichopungua miezi mitatu pamoja na faini.
Indonesia Unaweza ukatembelea fukwe na maeneo yenye vivutio mbalimbali nchini Indonesia; lakini uwe makini na swala la kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani kwani halikubaliki.
Vietnam Pamoja na mabadiliko mbalimbali kwenye utamaduni wa Vietnam, bado maeneo mengi hasa ya vijijini hayakubaliani na swala la kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani. Unaweza usilishuhudie hili hadi pale utakapotoka nje ya miji mikubwa kama vile Hanoi na Saigon.
Kwenye chuo kikuu cha zimbabwe, mwanafunzi anaweza kufukuzwa chuoni kwa kosa la kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani. Hairuhusiwi kubusu, kukumbatia au hata kukaa kimapenzi katika viunga vya chuo.
Kwa kupitia tovuti ya Egyptian Streets, mwanadada Farah anaeleza jinsi alivyokutana na wakati mgumu kumkumbatia au kumbusu mpenzi wake wa Misri waliekutana huko Ulaya.Ni wazi kuwa kanuni za Misri haziruhusu kuonyesha hisia za kimapenzi hadharani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.