Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Naamini unafahamu kuwa asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji. Lakini je wajua kuwa asilimia zaidi ya 75 za ubongo wa binadamu ni maji? Fahamu hili sasa.
 
Je wajua kuwa nywele za binadamu ni sehemu hai ya mwili? Nywele za binadamu zinaweza kuishi kwa miaka 3 hadi 7.
 
Ingawa mtoto mchanga napozaliwa meno yake yanakuwa bado hayajachomoza kwa nje, lakini yanakuwa tayari yameshaanza kuota kwa ndani miezi sita kabla ya kuzaliwa.
 
Kila figo yako moja ina vichujio takriban milioni moja vinavyochuja lita 1.3 za damu kila dakika na kupelekea kuzalisha lita 1.5 za mkojo kwa siku.
 
Inasemekana ni watu wachache pekee ndiyo wanaoweza kuchezesha masikio yao duniani. Je wewe unaweza? Ikiwa unaweza basi uko kati ya hao wachache.
 
Mwili wa binadamu una misuli kati ya 600 hadi 800. Pia inahitajika misuli 200 ili kuweza kupiga hatua moja.
 
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Leslie Vosshall kwenye chuo cha Rockefeller, ulibaini kuwa pua ya binadamu inaweza kubaini harufu tofauti takriban trilioni moja
 
Kiwango hiki ni tofauti na kilichokuwa kinafahamika mwanzo cha harufu 10,000. Je wewe unajua ulishanusa harufu ngapi? Kama unajua basi tuandikie hapo chini.
 
Inaelezwa kuwa ikiwa mwanaume hatonyoa ndevu katika maisha yake yote; ndevu zake zinaweza kukua na kufikia urefu wa mita tisa.
 
Mwili wa binadamu una misuli kati ya 600 hadi 800. Pia inahitajika misuli 200 ili kuweza kupiga hatua moja.
 
Inaelezwa kuwa binadamu anaweza kuishi siku 30 bila chakula; siku 3 bila maji; dakika tatu bila oksijeni. Je ulilifahamu hili kuwa unaweza kunywa maji tu bila kula na ukaishi siku thelathini?
 
Rekodi ya dunia ya mtu aliayeweza kukaa muda mrefu zaidi bila kulala iliwekwa na Randy Gardner ambaye alikaa siku 11 pekee. Inaelezwa kuwa ukikaa zaidi ya hapa utaanza kupata matatizo ya kiakili na kisaikolojia.
 
Back
Top Bottom