Nchi nyingi zimejizolea utajiri mkubwa kutokana na madini haya; pamoja na utajiri huu pia nchi nyingi zimesababishiwa uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na uchimbaji wa dhahabu.
Mwanakemia wa Hungary George de Havesy aliyeyusha tuzo za Nobel za wanafizikia wa Kijerumani Max von Laue na James Franck, ili kuzuia utawala wa Kinazi kuzitaifisha. Hata hivyo tuzo hizo za dhahabu ziliundwa tena upya baada ya vita.
Manahodha wengi wa kale walivaa hereni ya dhahabu ili wakizama majini na miili yao itakapookotwa ufukweni, basi hereni hiyo iuzwe ili igaramie garama za mazishi.
Huko dubai kuna ATM kwa ajili ya kutolea vitofali vya dhahabu. Je wajua kuwa utajiri huweza kuhifadhiwa kwa vipande au vitofali vya dhahabu? Basi huko dubai matajiri wanaweza kutoa vipande hivi kwenye ATM kama watoavyo pesa.

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.