Mwanasiasa wa Kirumi Gaius gracchus, kichwa chake kilihitajika kwa malipo ya dhahabu sawa na uzito wake. Hivyo atakayemuua na kupeleka kichwa chake angepewa dhahabu sawa na uzito wa kichwa hicho. Hata hivyo dhahabu hii haikulipwa kwa mtekaji kwa sababu alikijaza kichwa hicho madini ya risasi ili kiwe kizito zaidi.
Wanawake wa India wanavaa asilimia 11 ya dhahabu yote iliyoko duniani. Hiki ni kiasi cha zaidi ya kilichoko Marekani, Uswisi, Ujerumani na IMF zikijumuishwa kwa pamoja
Kipande au tofali kubwa zaidi la dhahabu duniani lina kilo 250. Tofali hili linamilikiwa na kampuni ya Mitsubishi, na linakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani 3,684,000.
Simu ya ghali zaidi duniani ya iphone5 imetengenezwa kwa dhahabu na ina thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 8. Simu hii pia imewekewa almasi nyeupe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.