Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

The youngest World Cup goalscorer in Spanish history is Gavi, who holds the record at 18 years and 110 days old. Gavi scored during Spain's 7-0 victory over Costa Rica on November 24, 2022.
 
Moto unaweza kukupa faraja wakati wa baridi Kali, ndio huo huo unaweza kukuchomea nyumba ukalala kwa jirani..

Chunga washauri wako.
 
Pneumonoultramicroscopicsilicovolcanoconiosis”

Hili ni jina moja, huu ni ugonjwa wa mapafu unaomtokea mtu baada ya kuvuta hewa yenye chembechembe za vumbi la ‘silica’
 
Sio wote wana dharau, kuna mtu pole yako juu ya kupaliwa kwake na kipande cha muhogo kaipata,
lakini kashindwa kuitikia ahsante kwa wakati, kwa sababu bado yupo kwenye tatizo lililofanya umpe pole..
Tuache hasira, tuwaelewe watu.
 
Kwenye madaftari tu ndo mshika mawili moja humponyoka.

Huku Uraiani watu wana kisu, hela,mfuko wa cement na sigara mdomoni na vyote vinafika.
 
Ukitaka heshima jifunze kuitoa hata kabla ya kuitwa mkubwa.

Waheshimu watu bila ya kujali hali zao, ukikuwa bila ya nidhamu utarudi nyumbani
 
Nikukumbushe tu....,

Watu wanaotamani uteseke wapo kwenye kundi la watu wanao kusifia Kila siku.
 
Kuna watu watahudhuria msiba wako, ili kuepusha maswali ya kwanini hushiriki matatizo ya wenzio..

Na sio kuguswa na kifo chako, Wapo hao!
 
Hii Afya tuliyokuwa nayo hakika ni Zawadi kubwa mno,
Kuna Binadamu wenzetu wanapitia mateso ya maradhi mno!
 
Hata MUNGU akikuletea mtu wa ndoto zako kama bado una maumivu, chuki na majeraha ya nyakati zilizopita bado utaharibu uhusiano huo..
JIFUNZE KUPONA.
 
Tuna walilia waliokufa na kuwadhihaki walio hai, hakika shukrani za binadamu zipo kwenye majuto.
 
Tunahangaika ili tuwe na kesho nzuri, lakini kesho ikifika, tunawaza tena kuhusu kesho nyingine nzuri zaidi..

Hebu jaribu kuiishi leo yako pia, halafu utaniambia...

Simple!..
 
Ukiona mtu hataki kabisa kumuumiza mtu elewa kabisa kuna namna aliyaishi maisha ya maumivu au alilelewa katika familia iliyojaa maumivu.
 
MIND -hutuongoza katika mipango mipya ya maisha mapya hivyo licha ya historia ama rekodi mbaya za maisha yetu ya nyuma, bado mind hutupa tafakuri ya plan mpya.
 
Wakati tunaendelea kupambana tusijaribu hata kidogo kuacha kuamini katika mapambano yetu.
Hatukuumbwa kusindikiza wengine ila kuzisindikiza historia na tuyakaribie mafanikio.
 
Msihi Mungu aonekane katika maisha yako, aondoe giza lililoko mbele yako nuru itawale na amani iwe ndani mwako.

Mlilie Mungu wetu juu ya hali yako unayoipitia sasa kiafya, kiuchumi, mahusiano au katika eneo lako la uhitaji akuimarishe.
 
Back
Top Bottom