Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Haijalishi unajisikiaje leo, inuka, vaa na ujitokeze mbele za watu ili upambanie hatma ya Maisha yako na familia yako. usikae kinyonge utanyongwa.
 
Tango ni tunda lisilo na ubaguzi japo halina umaalufu mkubwa kwenye jamii zetu,mwenye vidonda vya tumbo anakula, mwenye kisukari anakula, mgonjwa wa figo anakula maana halina potassium nyingi.
 
Vyakula vya moto sana au vya baridi sana hukereketa utando laini wa tumbo na huweza changia au kuwa chanzo mojawapo cha saratani, kwa hivyo ni muhimu kutumia vyakula vyenye halijoto ya wastani.
 
Tukiwapa msaada tusiende kuwatangaza popote,tusipige picha kwa ajili ya likes za mitandaoni..Utu over kitu..Twendeni tukawainue wenzetu wanatuhitaji.
 
Kila kitu kina thamani, na thamani ya kitu inatokana na mahali na wakati uliopo.Huenda Sukari ni tamu sana, lakini haifai wakati wa supu.
 
Moyo tuna ndoto zetu ila mpaka sasa hatuna mtaji, Sisi ni wale bila ya Mungu leo na kesho ingekuwa Aibu.
 
Kwanini tenga la nguo chafu huwa na matundu? Hii husaidia kupitisha hewa itakayo saidia kupunguza mazalia ya baadhi ya bacteria wanao ambatana na jasho la mwili, pia husaidia kupunguza harufu itakayo tokana na mazalia ya bacteria kwenye nguo.
 
Hakikisha kitu unachoendelea kumuomba Mungu ni Fedha na uzima, Kuhusu hawa walimwengu wewe Dili nao jinsi wanavyo Dili na wewe.
 
Jitahidi kulipa madeni unayodaiwa,Ipo hivi kila mwenye kudai anapo chukizwa kwa kutokulipwa deni lake basi wewe milango yako ya utafutaji ndio inakuwa migumu.LIPA DENI!
 
Pesa haimbadilishi mtu huwa ina kawaida wa kuonyesha uhalisia wa mtu usiouona kipindi hana.
 
Watu wenye akili kidogo hujituma ili tu wapate hela ya kula na kodi , mwerevu hufikiri kwa mapana ili apate njia ya kujiondoa jumla kwenye umasikini
 
Kizazi kinachorithi pesa bila maadili, mara nyingi hupoteza vyote. Kizazi kinachorithi maadili, kinaweza kujenga utajiri mara mbili zaidi
 
Back
Top Bottom