Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mh [HASHTAG]#GoodluckMlinga[/HASHTAG] amezidi kutetea hoja yake ya kuwa wasanii waliofanya vizuri na kuiwakilisha nchi nje vizuri, kupewa heshima kama kujengewa sanamu na baadhi ya mitaa na barabara kupewa majina yao. . . Kipindi cha nyuma Mbunge huyo alisimama Bungeni na kusema kwa namna msanii [HASHTAG]#DiamondPlatnumz[/HASHTAG] anavyoiwakilisha nchi vizuri kimataifa anastahili kujengewa sanamu, na kupendekeza ikibidi sanamu la askari posta Dar es Salaam liondolewe na kuweka hilo la [HASHTAG]#Diamond[/HASHTAG] . . . [HASHTAG]#GoodLuck[/HASHTAG] “Na sikumtaja Diamond pekee, niliwataja wasanii wengi kama wakina Mr Nice ambao wameiwakilisha Tanzania sana nje lakini mpaka leo hii wamepotea hawana alama, inakuwa hawawezi kuwahamasisha wasanii wengine, lakini tunapoweka alama kila msanii anapofanya vizuri tunahamasisha wengine na ndiyo utaratibu katika nchi za wenzetu,” ameiambia Habari Xtra ya Times Fm . . Na kuongeza“Kuna mchezaji mmoja wa mpira alitoka Kenya (Victor Wanyama) kuja Tanzania siku ya pili alipewa mtaa, sasa vile vitu ndio tunatakiwa tuvifanye kwa wasanii wetu wanaoibeba nchi. Sasa wewe fikiri mtu katoka nje ambaye anawakilisha nchi nyingine tunampa mtaa, lakini kwetu ni msanii gani alishawahi kuacha alama hata akapewa Barabara, hakuna!!!,” . . . JE UNAMUUNGA MKONO MBUNGE HUYU AU UNAMPINGA?? . TOA MAONI YAKO HAPA
20066946_480455365646315_8501916319669551104_n.jpg
 
Msanii Alikiba ambaye siku za karibuni aliahidi kuachia ngoma yake mpya amefunguka na kusema baada ya kuachia ngoma hiyo inayosubiriwa na mashabiki zake kwa hamu atatambulisha wasanii walio chini ya 'Label' yake Kings Music. Alikiba amesema kwa sasa anawajenga hao wasanii waliopo chini ya uongozi wake huo ili waweze kufanana na yeye kwa mambo mengi na waweze kupata mafanikio kupitia muziki ambao wanafanya. "Nina label yangu inayofahamika kama 'Kings Music' lakini naweza kusema haijaanza kufanya kazi kwani toka nimerudi na kusimama kwenye muziki sijawahi kutoa msanii kwenye label yangu lakini saizi baada ya kutoa wimbo wangu mpya nitaanza kutoa ngoma kutoka kwa wasanii wangu kwani maandalizi yameshafanyika na videos tushafanya, ngoma ziko sawa na wasanii wenyewe wako vizuri. Nimewaanda wasanii wangu jinsi ambavyo mimi nipo nataka na wao wawe hivyo hivyo, wawe watu wa watu, wapendwe na watu, wawe na mashabiki wa kutosha yaani mimi nambadilisha mtu kwa lengo zuri" alisema Alikiba Alikiba anasema muda wowote ule anaweza kuachia kazi hiyo mpya kwani sasa kilichobaki ni kusema siku gani kazi hiyo itaachiwa kwani kila kitu kimeshakamilika hivyo anasubiri siku tu waweze kuachia kazi hiyo, ambayo inaonekana kusubiriwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa Alikiba. . . TOA MAONI YAKO HAPAView attachment 544742
Liked
 
Back
Top Bottom