Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

POSITIVE MIND VIBE QUOTES


[emoji617]Dharau haziwezi kuwa na faida kwa mwenye dharau bali kwa anayedharauliwa. Anayedharauliwa hawezi kupata faida ya kudharauliwa akimdharau anayemdharau, mana wote watakuwa na dharau. Uzuri wa kudharauliwa ni kwamba humfanya Mungu kukuinua zaidi ya anayekudharau mana asipofanya hivyo ni Mungu ndiye atakuwa anadharauliwa sio tu yule anayedharauliwa mana Mungu wetu ni mshindi na ametuumba kwa mfano wake. Haloo, naomba ukumbuke Mungu ni mchapa kazi kwa Maarifa na hekima kwahiyo acha watu wakudharau kwa kitu ambacho unakifanya kwa maarifa na hekima, wewe PIGA KAZI,hesabu dharau kama BARAKA kwako.


[emoji617]Sisi wote ni binadamu na tunapitia vipindi tofauti katika maisha kama shida na matatizo mbalimbali ni kawaida kutokea lakini hivi vyote kuvipa muda kuviwaza kwa jinsi vilivyo hasi ni kuvikuza na kuvitengenezea makazi ndani yetu. Vikija tukubali kuja lakini tusikubali viishi ndani yetu hata siku moja. Mambo yote ambayo yanafanya Moyo wako kuteseka ni USAFIRI WA SHETANI kuja kukuangamiza. Chukua usafiri mwingine wa Kuvitawala hivi kwa UPENDO na KUVISEMESHA kwamba ni sawa kuja lakini havina makazi ndani yako.


[emoji617]Ukiwa na uongo ambao unadhani utakuwa ni kweli utaficha hata kweli uliyokuwa nayo sasahivi. Kuna jambo unafanya lifanye kwa ukweli na sio lionekane la ukweli wakati unadanganya, hii inaweza kukufanya hata kupoteza yale machache ya ukweli uliyokuwa nayo.

[emoji617]Kuna kuamka asubuhi na kujuta unapotoka mana hata inawezekana usiku ulikuwa unajisemesha bora kukuche, lakini nikwambie kitu ewe Mkristo na Muislamu mwenzangu ABRAHAMU katika Biblia alikuwa na imani kwamba Kunasiku atakuwa na familia yake na uzao wake lakini kabla ya kumpata Isaka Mungu alimwambia Uzao wake utakuwa kama mchanga wa Bahari, alimwambia Uzao wake Utakuwa kama nyota angani. Wewe leo hii unalala njaa au unalala sehemu ambayo hairidhishi lakini nawe kunasiku utakuwa zaidi ya matamanio ulikuwa nayo, kuna siku utakuwa na shibe zaidi ya njaa ambayo unayo leo, utakuwa na utajiri zaidi ya bajeti kali ambayo unayo kwa siku au mwezi au mwaka, Kumbuka Ayubu alivojaribiwa na shetani alipotezewa kila kitu lakini baada ya kushinda majaribu Alipata Mara mbili zaidi ya vya kwanza alivyokuwa navyo (Ayubu alionesha nidhamu,utii na Imani kubwa sana). Wewe kwani ni nani ambaye Mungu anakupa pumzi ya kuona changamoto za maisha na asikupe nguvu ya kuzishinda, wote tusimame na tuwe washindi. INAWEZEKANA.




Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Busara hizo shemeji. Well said ndugu. Tupendane, tuvumiliane lakini pia tuwe wasikivu. Mwenzako akisema kuwa jambo fulani linamkwaza, si vibaya ukimsikiliza badala ya kujifanya wewe ndiyo unajua kila kitu. Mikwaruzano ya hapa na pale itakuwepo lakini tukiwa wakweli na kukanyana kwa staha, uzi huu utaendelea kuwa stress free na utaendelea kuwa kimbilio la wengi. Na lengo kuu bado ni lile lile: TOA LIKES POKEA LIKES.
 
Hunter hilo swali ni la msingi sana katika maisha.
Big up sana hunter.
 
*[emoji42][emoji47]WAKE UP CALL[emoji337][emoji338]*


Kumbukumbu nzuri kwa watu kuhusu maisha yako na maisha ya wengine hautaitengeneza kwa kununua magari mazuri, kujenga nyumba nzuri, kutoa watu out kila weekend ila utaitengeneza kwa kuwasaidia kuwaachia kitu flani katika akili zao. Gari linaweza kuharibika wakakusahau, nyumba inaweza kuharibika au hata kubomoka wakakusahau, kuwatoa out wanaweza kusahau, kuwapa hela zitaisha na hawatakukumbuka. Wape maarifa na waoneshe upendo hivi vitakaa katika AKILI NA MIOYO yao, kifupi gusa maisha yao katika hivi vitu.

Hawatakusahau mpaka Mungu awachukue licha ya hivyo lazima watawahadithia na watoto wao na watoto wao watawahadithia watoto wao na vizazi kwa vizazi.

UKITENDEA WATU WEMA WEMA WAKO UTAKUWA FASIHI SIMULIZI KWA KILA MMOJA HATA KATIKA VIZAZI VYAO.



Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Wenye vi-okra wamepigwa marufuku kusema "Naliamsha dude". Naona wamekuja na "Usiniamshie kadude" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji124] [emoji124] [emoji124] anajibu maombi...anajibu maombi...[emoji94] [emoji445] [emoji444] [emoji445] [emoji444] [emoji443] [emoji442]
 
POSITIVE MIND VIBE QUOTES

[emoji617]Kukosa msimamo na maisha yako ni kuacha maisha yako kuwa ya kuridhisha kila mmoja. Maisha ya utumwa ndipo yanapoanzia na hii tabia huwa inafanya watu kuwa watumwa kwa watu wengine bila hata kujua. Kumridhisha mtu unatumia akili na nguvu kwasababu ni lazima ufanye kitu ambacho kinaendana na tabia ya kila mtu, sasa kitakachofanyika ni kwamba muda unakuja kujitambua kwamba unatakiwa kujiridhisha mwenyewe unakuta kwamba umeshajenga tabia ambayo inakuwia vigumu wewe kujitambua na kuanza kufanya mambo yako.


[emoji617]Ajira sio mbaya ila ubaya unaokuja ni kwamba kutafuta ajira kumevunja Akili za sisi vijana kuwaza kwamba tunaweza kuungana na kufanya jambo flani, ni wachache sana ambao wegundua hilo na kuweza kujumuika pamoja bila kusubiri ajira. Akili zikiwa zimelenga kuhusu kufanya kazi za watu kunaasilimia ndogo sana kuwaza kuhusu kufanya mambo yetu.


[emoji617]Kukosa busara ni kupinga kitu ambacho hujui kusudi la mwanzilishi wa hicho kitu, yani mawazo yako unaona ni sahihi kama mwanzilishi au ndiye mtendaji wa hilo swala. Uliza kwanza kusudi la jambo flani ndipo upinge au ukubaliane kama hujaelewa kinachofanyika.

[emoji617]Dalili za umasikini zinaonekana kwenye hayaonekani lakini yakizidi kwa matendo huonekana mfano ;
-Wivu
-Masengeny'o
-Uchoyo
-Tamaa
-Chuki n.k
Mafanikio ni kanuni wala hauwezi kusema kitu flani ambacho ni kibaya kinaubaya kidogo, ubaya ni ubaya hata kama uipande na ukweli utajitenga. Mafanikio ni kweli.




Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…