Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukitaka mambo mazuri katika maisha yako lazima ukubaliane kuweza kufanya maamuzi magumu. Usiwe mtu wa huruma sehemu ambayo haziitaji kuwa na huruma.Maisha mabovu huwa tunajitakia
sisi wenyewe.Unakuwa na marafiki ambao sio sahihi unasema nawavumilia lakini huyo rafiki yeye kumbuka havumilii kukuambukiza tabia ambazo sio sahihi, ukiwa mfungwa wa ujinga wa mtu flani utakuwa mmoja wa wajinga. Lazima ifike wakati kwamba uangalie sehemu ambayo unaenda uache kufanya maamuzi ambayo hayakupeleki mbali, maamuzi ambayo hayakupi picha nzuri ya baadae. Maamuzi magumu ni pamoja na

1. Kuhakikisha kwamba mwaka huu kama uko sehemu ambazo sio sahihi katika mitandao na unapata mawazo ambayo hayana msaada wowote katika maisha yako ujitahidi kuyaondoa mfano Unakuwa na makundi mengi ambayo ukisema upitie ujifunze kitu hakuna hata moja ambalo unalipata zaidi ya kusoma jumbe za kawaida na kuondoka yani group lenye majadiliano ambayo hayaongezi kitu katika maisha yako toka mwaka umeanza mpaka unaisha ni group la kukimbia. Hapa wengi watasita sana na wengi wataona sio sahihi lakini Kaa jitafakari na angalia unamuda gani na hela yako ya Mb toka mwaka uanze zimekuongezea nini? Chukua maamuzi.


2. Chukua maamuzi ya kuachana na marafiki ambao wao kwao maisha ni kulalamika, kuwa na matumizi mabovu ya hela na kuiga maisha ya watu wengine. Usiseme usela au ujamaa, hakuna ujamaa wa kuwa na hali ngumu ya maisha wote kwapamoja wakati mko zaidi ya mtu mmoja, kutakuwa na tatizo kama mko zaidi ya 2 alafu mnalalamika kwamba maisha yanabana au maisha ni magumu au magufuli kabana alafu kila mmoja anaujuzi flani.Unapata wapi hela ya kupata pombe, sigara n.k kwanini hiyo nguvu ya kupata hela za hivyo vitu ukahamisha kisela kama vijana tunavyosema ili msaidiana kubadilisha maisha yenu? Usela wa kujitoa out kwa 100,000/= au zaidi kwa siku alafu mnakuja kusema maisha magumu hapo kunatatizo ndugu zangu, hiyo hela vijana wawili hamjaanzisha biashara ya chips au kuuza mishkaki taratibu? .




Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
POSITIVE MIND VIBE QUOTES

[emoji617]Kukosa msimamo na maisha yako ni kuacha maisha yako kuwa ya kuridhisha kila mmoja. Maisha ya utumwa ndipo yanapoanzia na hii tabia huwa inafanya watu kuwa watumwa kwa watu wengine bila hata kujua. Kumridhisha mtu unatumia akili na nguvu kwasababu ni lazima ufanye kitu ambacho kinaendana na tabia ya kila mtu, sasa kitakachofanyika ni kwamba muda unakuja kujitambua kwamba unatakiwa kujiridhisha mwenyewe unakuta kwamba umeshajenga tabia ambayo inakuwia vigumu wewe kujitambua na kuanza kufanya mambo yako.


[emoji617]Ajira sio mbaya ila ubaya unaokuja ni kwamba kutafuta ajira kumevunja Akili za sisi vijana kuwaza kwamba tunaweza kuungana na kufanya jambo flani, ni wachache sana ambao wegundua hilo na kuweza kujumuika pamoja bila kusubiri ajira. Akili zikiwa zimelenga kuhusu kufanya kazi za watu kunaasilimia ndogo sana kuwaza kuhusu kufanya mambo yetu.


[emoji617]Kukosa busara ni kupinga kitu ambacho hujui kusudi la mwanzilishi wa hicho kitu, yani mawazo yako unaona ni sahihi kama mwanzilishi au ndiye mtendaji wa hilo swala. Uliza kwanza kusudi la jambo flani ndipo upinge au ukubaliane kama hujaelewa kinachofanyika.

[emoji617]Dalili za umasikini zinaonekana kwenye hayaonekani lakini yakizidi kwa matendo huonekana mfano ;
-Wivu
-Masengeny'o
-Uchoyo
-Tamaa
-Chuki n.k
Mafanikio ni kanuni wala hauwezi kusema kitu flani ambacho ni kibaya kinaubaya kidogo, ubaya ni ubaya hata kama uipande na ukweli utajitenga. Mafanikio ni kweli.




Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
Liked
 
Sema shemeji. Hata ma-great thinkers huwa wanapita pita huku. Dada anaendeleaje na Malaria yake?
Anaendelea vizuri,tatizo dadaako anaipenda ajira kuliko mimi.Likizo ya ugonjwa aliyo pewa ilikuwa bado siku nne ziishe, ameamua kwenda kuzimalizia kazini[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
*POSITIVE MIND VIBE QUOTES*.


[emoji617]Usiogope changamoto lakini changa akili yako changamoto zikuogope.

[emoji617]Uzuri wa kuni hauko nj'e ya kuni mbali ni ndani ya kuni yenyewe.

[emoji617]Uzuri wa mtu haupimwi na aina ya mavazi au aina ya maisha anayoishi bali uzuri wa mtu unapimwa kwa kufanya mambo ambayo wengi wanaojiona wazuri hawawezi kuyafanya. Kiufupi uzuri wa mtu uko ndani ya tabia ambayo wengi huwa hawana uvumulivu wa kuistahimili kuifanyia kazi.

[emoji617]Uzuri wa ndoa haupimwi kwa uzuri wa harusi ilivyo bali ni kwa njisi bibi na bwana harusi walivyo ndani yao.

[emoji617]Uzuri wa mafanikio haupimwi kwa mangapi umejifanyia wewe mwenyewe ila unapimwa kwa mangapi umefanyia wengine ambao hawana uwezo wa kujifanyia hata chembe ya wewe uliyethubutu kuwafanyia kitu wao.


[emoji617]Uzuri wa heshima haupimwi kwa shikamo ila unapimwa namna ulivyoweza kutumia hekima yako kwa watu wengine.




Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
atakaye sikia na asikie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*GOOD NIGHT[emoji281][emoji283][emoji279][emoji42]*


*[emoji42][emoji47]WAKE UP CALL[emoji337][emoji338]*


Kumbukumbu nzuri kwa watu kuhusu maisha yako na maisha ya wengine hautaitengeneza kwa kununua magari mazuri, kujenga nyumba nzuri, kutoa watu out kila weekend ila utaitengeneza kwa kuwasaidia kuwaachia kitu flani katika akili zao. Gari linaweza kuharibika wakakusahau, nyumba inaweza kuharibika au hata kubomoka wakakusahau, kuwatoa out wanaweza kusahau, kuwapa hela zitaisha na hawatakukumbuka. Wape maarifa na waoneshe upendo hivi vitakaa katika AKILI NA MIOYO yao, kifupi gusa maisha yao katika hivi vitu.

Hawatakusahau mpaka Mungu awachukue licha ya hivyo lazima watawahadithia na watoto wao na watoto wao watawahadithia watoto wao na vizazi kwa vizazi.

UKITENDEA WATU WEMA WEMA WAKO UTAKUWA FASIHI SIMULIZI KWA KILA MMOJA HATA KATIKA VIZAZI VYAO.



Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
Amen!
 
*Yafahamu mambo manne yatakayokupa motisha na kukuamsha kufikia mafanikio unayoyataka siku ya Leo.*

==> Ulizaliwa kwa kusudi maalumu. Mungu amekuumba ili uje kutimiza kusudi Fulani. Haijalishi ulizaliwa katika mazingira gani. Mungu aumbi mitumba, Mungu aumbi vitu vya ovyo ovyo. Wewe ni tunda zuri LA uumbaji wa Mungu.

==> Umezaliwa mshindi kwani wakati unatungwa mimba, ulishindana na watu zaidi ya milioni thelathini (30), lakini ulipatikana na ukazaliwa wewe. Wewe ni mshindi.

==> Kila mtu anakitu cha tofauti ndani yake. Hakuna anayeweza kuandika kitabu kizuri kama wewe. Hakuna anayeweza kuimba vizuri kama wewe. Hakuna anayeweza kuhamasisha vizuri kama wewe. Hakuna anayeweza kupiga vizuri ala za muziki kama wewe. Hakuna anayeweza kucheza mpira vizuri uwajani kama wewe. Hakuna anayeweza kuhubiri vizuri kama wewe. Hakuna anayeweza kuanzisha kampuni yenye brand nzuri na kubwa kama wewe. Anza sawa kufanya maajabu. Wewe ni wa pekee. Wewe ni special.


==> Usisubiri watu wengine waje kukwambia unaweza, anza wewe kujiambia kwamba unaweza. Isikilize ile sauti iliyo ndani mwako inayokwambia kwamba unaweza. Ukisubiri watu wengine waje kukwambia kwamba unaweza utachelewa sana. Mafanikio daima uanza na wewe. Mafanikio yapo mikononi mwako.

See you at the top



Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Back
Top Bottom