Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Thanks my dear brother
 
Asante mkuu na karibu tena huku!
 
POSITIVE MIND VIBE QUOTES


[emoji617]Kila siku ni fursa ndomaana hauwezi kukuta jana ikafanana na leo na siku zinabadilika kukutia moyo kwamba kama jana ulikosa au ulipata kidogo usikate tamaa kuna kesho inakupa matumaini ukiweka juhudi.Ukiona zinafanana jua wewe ndiye uliyezifananisha.


[emoji617]Akili ya ushindi ni kutumia fursa inayonekana sio fursa kuwa fursa, kutumia muda unaoonekana kwamba hautoshi kwa visingizio kuweza kutosha,kutumia mapungufu yako kama nguvu ya kukuinua zaidi, kutumia kidogo chako kukuletea vikubwa, kutumia hali ya maisha ya familia yako ambayo haikuridhishi kuwa kama kichochea cha kuipeleka unapopenda.

[emoji617]Usijute kwa hali ya maisha ambayo unayo sasahivi ila jiulize Mungu alikupa Muda wa kulalamikia matatizo au muda wa kumwomba yeye akusaidie nguvu za kuyashinda? Ugumu upo lakini haina maana Mungu atakuacha uteseke Maisha yako yote kunasiku atakupa ushindi.

[emoji617]Mateso yako ya leo ndiyo faraja yako ya kesho kama hutakata tamaa kupigania unachokiamini katika maisha yako.



Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
*POSITIVE MIND VIBE QUOTES*.


[emoji617]Usiogope changamoto lakini changa akili yako changamoto zikuogope.

[emoji617]Uzuri wa kuni hauko nj'e ya kuni mbali ni ndani ya kuni yenyewe.

[emoji617]Uzuri wa mtu haupimwi na aina ya mavazi au aina ya maisha anayoishi bali uzuri wa mtu unapimwa kwa kufanya mambo ambayo wengi wanaojiona wazuri hawawezi kuyafanya. Kiufupi uzuri wa mtu uko ndani ya tabia ambayo wengi huwa hawana uvumulivu wa kuistahimili kuifanyia kazi.

[emoji617]Uzuri wa ndoa haupimwi kwa uzuri wa harusi ilivyo bali ni kwa njisi bibi na bwana harusi walivyo ndani yao.

[emoji617]Uzuri wa mafanikio haupimwi kwa mangapi umejifanyia wewe mwenyewe ila unapimwa kwa mangapi umefanyia wengine ambao hawana uwezo wa kujifanyia hata chembe ya wewe uliyethubutu kuwafanyia kitu wao.


[emoji617]Uzuri wa heshima haupimwi kwa shikamo ila unapimwa namna ulivyoweza kutumia hekima yako kwa watu wengine.




Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Endelea mkuu. Nakusikiliza!
 
Well said
Big up
 
Pokea like
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…