Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tubarikiwe sote Mkuu SHIMBA YA BUYENZE. Nafurahi kuwepo kwenye huu uzi nasikitika tu sikuja mapema pamoja na nilikuwa nauona lakini nilikuwa naupotezea.

Kuna watu hapa wastaarabu na waungwana sana na wanaonyesha jinsi wanavyokujali, kukuheshimu na kuthamini uwepo wako katika uzi huu. Na ni kweli umeniwekea likes nyingi sana na bado unaniwekea, niwe mkweli tu kwamba nilikuwa nimekuweka kwenye list yangu ya watu niliowaignore lakini nimekuondoa huko tangu Jumamosi Mkuu.

Shukrani sana Mkuu kwa uelewa wako mkubwa. Tupo pamoja Mkuu na ahsante sana.
BAK mimi naomba nikushukuru kwa uungwana wako. Ni ngumu sana kwa mwanadamu kuomba msamaha au kukubali kitu ambacho alikikata.
Huu uzi umetupa nafasi nyingine na sababu ya kuwepo JF. Tumegundua kuna maisha ndani ya JF. Watu wana furahi wanacheka tumekuwa na marafiki ambao hatujawahi kuonana. Wewe mwenyewe ukipotea lazi uuliziwe umekwenda wapi.
Bro ubarikiwe sana Mungu azidi kukupa amani kuwepo humu.
 
Back
Top Bottom