Uzi maalum wa kuwakumbuka Walimu waliotufundisha kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu

Uzi maalum wa kuwakumbuka Walimu waliotufundisha kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu

Waliosoma mbeya AIRPORT pr. Wanajua moto wa mwalimu KANYIKA kuanzia chekechea mpaka namaliza cjawahi jumuona akicheka

Fimbo zake mpaka Leo zinajirudiq kichwani mwanguu


Anyway popote alipo madqko yake
Walimu wengine tunawakumbuka kwa mema waliyotutendea. Lakini wapo wengine tunawalaani kwa mateso waliyotufanyia tukiwa chini ya mamlaka yao. Hao ni pamoja na huyo Mwalimu wako katili.
 
Tukiachana na Mpwayungu Village ambaye usiku na mchana yeye ni kuwasakama walimu, tupo sisi wengine tunaoheshimu na kuthamini mchango wao kwenye maisha yetu ya kila siku.

Walimu wangu wa chekechekea kuna Teacher Mary, Umoja Primary School.
Mama Stambuli, mama mzazi wa Azza, amenifundisha pia prep Umoja.

Mama yake Shikunzi, Anna Mgaya, amenifundisha Primary Umoja. Mr. Lohah alikuwa mwalimu wetu mkuu.

Sisimba nimefundishwa na Richard Kasela mtu mwenye vipaji vyake lukuki, Mwaisaka mkali wa hisabati.

Mtawa na Msuya ndio walikuwa walimu wakuu. Muchuruza, Nyandindi, Mapunda, Mwaisumo, mwl Matthew (mama yake William Mpangala), mwl Benard (mama yake Edmund Ntalugela), mwl Chang'a na wengine heshima kwenu.

Walimu wangu wa sekondari hasa Yisambi Reka Ntipoo, gwiji la hisabati you are the best teacher ever. Mwl Mageta mwalimu wangubwa Commerce na Book Keeping ulinijengea msingi imara wa mimi kuwa hivi nilivyo leo, Mwalimu Mwangoka alikuwa mwalimu mkuu pale Meta. Miss Jackson (Mrs Alinani Mwakalindile a.k.a Mama Niti) ulinifanya niijue vizuri Geography na nitamaniniizunguke dunia. Namshukuru Mungu nimeenda Australia, America Kaskazini (Canada [emoji260] na USA [emoji631]) sijaenda Mexico tu, nimezurura America Kusini, Asia, Ulaya, na Africa nyumbani.

Chuo pale Doriye ndio alikuwa principal wetu. Cleopa, madame Irene, Ndasa na wengine wengi nawashukuru sana. Shukrani na heshima kwenu.

Mungu awabariki sana walimu wote wa Tanzania
Dah! Wwe Jamaa unakumbukumbu nzuri sana kuwakumbuka walimu wote hao,barikiwe sana! Mi mwenzio walimu ambao wako kichwani mwangu ninao wakumbuka ni watatu wa primary, Mwalimu Mwaka, Mwalimu Imamu na Mkuu wa shule Mwalimu Sabuni!!
 
Back
Top Bottom