Uzi maalum wa machimbo makali ya bei poa kwa ajili ya Honeymooners na wapenzi wanaohitaji faragha

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001


Privacy ama kujitenga ni jambo jema sana. Wengi hupenda kujitenga mara baada ya kufunga ndoa, hutafuta sehemu ya uficho kwa ajili ya kwenda kutafakari safari yao nzima ya maisha. Watahitaji sehemu nzuri yenye utulivu na kila kitu kizuri.

Wengi hatuna taarifa au maarifa ya kuyafikia haya machimbo makali ya bei rahisi lakini leo nitakupa mtonyo kidogo ili siku ukitaka mafaida usipate shida.


Fuatana nami
 






Hili chimbo ni Beach Front, unapata kijumba chako kamili, choo, jiko, sebule, chumba cha kulala na kighorofa cha kupungia upepo mwanana wa bahari.

Raha zote hizi unapata kwa shilingi 100,000 tu kwa siku, huku ukiendelea kupata Internet ya bure yenye kasi ya ajabu.

Sehemu ni salama na inafikika kirahisi.
Kwanini uishi kwa kujibana bana?

Hapa kwa wapenzi wa kukaa bila nguo (nudists) ni mahali sahihi. Ukipewa funguo, umepewa Paradiso yako.
 
Kweli Tarime ni kuzuri
 


Kwanini usije kutulia kwenye hii pepo ndogo? Pepo hii yenye vyumba vitatu vya kulala ni muafaka sana kwenu, hasa mkitaka kutoka kwa mapumziko kama familia.

Pia washikaji na pisi zenu kali, mnaweza kuamua kujitoa out mkaingia Ijumaa baada ya kazi, mkatoka jumapili usiku.

Njoo uiponye roho yako kwa shilingi 100,000 tu kwa siku.

Bustani nzuri zenye ndege, na vipepeo, zitakusahaulisha machungu yote ya mauzo ya bandari.
 
Inapunguza hadi machungu ya mauzo ya bandari?Hiyo ni kiboko zaidi ya kifimbo.🤔
 
Umaskini mbaya nyie dah. Hebu fikiria demu wako kaja kugongewa kwenue mji kama huu, atarudi kwako afuate nini tena?
 
Napenda sana bustani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…