Uzi maalum wa machimbo makali ya bei poa kwa ajili ya Honeymooners na wapenzi wanaohitaji faragha

Uzi maalum wa machimbo makali ya bei poa kwa ajili ya Honeymooners na wapenzi wanaohitaji faragha

Screenshot_20230808-081251_Lite.jpg
 
Hapa ni wapi? Nataka nifike kisha nimtumie picha mwalimu wa Maths nimuulize kwani hapa ni wapi?
View attachment 2711524
View attachment 2711525View attachment 2711526
Kwanini usije kutulia kwenye hii pepo ndogo? Pepo hii yenye vyumba vitatu vya kulala ni muafaka sana kwenu, hasa mkitaka kutoka kwa mapumziko kama familia.

Pia washikaji na pisi zenu kali, mnaweza kuamua kujitoa out mkaingia Ijumaa baada ya kazi, mkatoka jumapili usiku.

Njoo uiponye roho yako kwa shilingi 100,000 tu kwa siku.

Bustani nzuri zenye ndege, na vipepeo, zitakusahaulisha machungu yote ya mauzo ya bandari
.
 
View attachment 2711517

Privacy ama kujitenga ni jambo jema sana. Wengi hupenda kujitenga mara baada ya kufunga ndoa, hutafuta sehemu ya uficho kwa ajili ya kwenda kutafakari safari yao nzima ya maisha. Watahitaji sehemu nzuri yenye utulivu na kila kitu kizuri.

Wengi hatuna taarifa au maarifa ya kuyafikia haya machimbo makali ya bei rahisi lakini leo nitakupa mtonyo kidogo ili siku ukitaka mafaida usipate shida.

View attachment 2711518
Fuatana nami
Hili chimbo lipo wapi?
 
Umasikini sio hali ya kukosa vitu, mali au fedha, Umasikini ni mindset.

Kufuatilia maisha ya wengine ni umasikini.
Kuwaombea mabaya wengine ni Umasikini
Kuwaroga wengine ni umaskini
Kutotenda mapenzi ya Mungu pia ni umasikini mkubwa zaidi
 
Back
Top Bottom