Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Mkuu pole sana, hata RAQEEB BUS , sijui kwakuwa wamekosa abiria kipindi hiki cha korona, ukituma percel wanachukua kimiya kimiya anayepokea wanamtolea hasira analipia siti kwa bahasha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Taratibu jamani.
Mbona huwa hupendi kushindwa ? Sometimes I hate the way you react to your colleagues.
Kama ni age factor ni ya kwako sio ya kwetu.....
Kama ni elimu ni ya kwako sio ya kwetu....
Kama ni pesa ni zako pia...
Kama ni dharau ni zako vile vile.

Respect people and take my comment seriously.
 
Kwani kutuma barua kwa posts kwa EMS au Ile DHL Ni Bei gani..maana uzuri wa Basi mzigo inafika in express way...unatuma leo inafika leo..na kumbuka wanapesa leseni na TCRA
 
Wakuu natumaini mko poa

Hapo awali nilikuwa napiga biashara ila sikukata leseni wala kitambulisho cha mjasiriamali. Ila kuna siku mapolisi walilengeshwa wakaja kunipiga hela (fine) kwa kigezo sina leseni na nina operate masaa ambayo hayajaidhinshwa kwa mujibu wa leseni ya biashara niliokuwa naifanya maana ilibidi kufungua kuanzia saa 9 alasiri.

Hii situation ikanifanya nika-process leseni ila ule mchakato sikuumalizaga, niliishia kuchukua application form ya pink ya manispaa kisha baada ya kuijaza wakaniambia niende TRA kupata Tax Clearance. TRA nilienda kweli nikapewa form flani yenye control number nikaambiwa nikalipie laki 1 baada ya mahojiano mafupi juu ya biashara.

Kimsingi ile laki sikulipa maana ilikuwa december ambapo nikaambiwa ntarudi tena mwezi wa 3 kulipa tena. Nilichekecha akili nikaona kile kitu ni kama kulipia kiingilio cha disko saa 12 kasoro alfajiri. Nikasema ntalipa mwezi wa 3 ili kama ni charge ya mwaka mzima basi iwe hivyo.

Kwa kifupi ile biashara nimeifunga sasa nawaza je, kwa hiyo scenario mamlaka ya mapato itakuwa napaswa nikajisalimishe tena na kuwaambia biashara nimefunga na watanidai zile hela ambazo sijalipia kwenye ile form au nipotezee niendelee na harakati zingine nile kobis?

NB: Mchakato wa leseni sikuukamilisha maana sikurudi tena manispaa nilibaki na form yao tu ya kuomba leseni na ile Tax clearance form ya TRA ila nilicholipa ni hela za usafi wa mazingira kwa serikali ya mtaa tu.
 
Tax clearance hailipiwi kinacholipwa ni malimbikizo ya kodi kama ulikuwa nayo isitoshe kama biashara unasajili upya ni bure kabisa
 
Umeenda hospital ukalipia pesa ya kumuona Dr hukwenda ukakimbia!!!
Unaweza kwenda kuchukuwa majibu ya ugonjwa wako?Dr anaweza kuwa na majibu ya ugonjwa wako!?
 
Unadaiwa laki 1 na penati ya elfu 75 kila mwezi uliozidisha. Wahi haraka ukamalizane nao kabla deni halijawa mlima.

Mkuu kwani wana taarifa zake zozote? Endapo nimemuelewa vizuri bingwa kule TRA alichukua form tu akachikichia mitini.

Ni kama vile haina madhara ikiwa tu hawana taarifa zake zozote.
 
Mkuu kwani wana taarifa zake zozote? Endapo nimemuelewa vizuri bingwa kule TRA alichukua form tu akachikichia mitini.

Ni kama vile haina madhara ikiwa tu hawana taarifa zake zozote.
Alienda TRA wakampa fomu yenye control number ili akalipe laki 1 baada ya mahojiano mafupi.

Ina maana alifanyiwa makadirio ya kodi. Labda kama alikadiliwa 0.00 Tsh kwa kuwa alienda mwishoni mwa mwaka. Lakini laki 1 inasomeka kwenye system.
 
Umeenda hospital ukalipia pesa ya kumuona Dr hukwenda ukakimbia!!!
Unaweza kwenda kuchukuwa majibu ya ugonjwa wako?Dr anaweza kuwa na majibu ya ugonjwa wako!?
sidhani kama situation zina match ila ni kwamba nili convert TIN toka driving Licence na kuwa ya biashara kisha nikafanyiwa mahojiano mafupi tukafikia kwenye form flani ambayo walitaka nikalipe laki maana ndio biashara imeanza sijaanza kukadiriwa rasmi.

Mi kwa kuona ni mwisho wa mwaka nikaona siwezi lipia biashara december laki hela ya mwaka mzima halafu mwezi wa 3 nilipe tena laki ingine ya mwaka mzima.

Nikauchuna hadi mwezi wa 3 ambapo pia sikulipa baada ya mlipuko wa Corona.

Sasa hapo ndio napanga nipotezee au nifanyaje ili kuepuka soo kama kutakuwa na kufuatiliwa
 
Ile control number unatoka kwenye mfumo kwahyo Kama ujalipa hyo laki moja Deni bado linasoma nakila mwisho wa mwezi system inakupiga penality ikifika mwezi wa tatu itajiongeza tena kwa sababu Kodi TRA unalipa kwa awamu tatu kwa mwaka kwahyo ukija kufika desemba bila kulipa utakuta Deni ni mlima sio Tena kichuguu.
 
Mkuu kwa uelewa wangu baada ya mahojiano walikuprintia fomu ya malipo ya laki moja uende ukalipie benki au kwa wakala siyo? Kama ni hivyo walishaingiza taarifa zako kwenye mfumo wa TRA. Ilitakiwa usiende kabisa au ujifanye umekuja kupata taarifa za nini ufanye ili upate leseni. Kwa kifupi unatakiwa kulipa hiyo laki pamoja na penati na uwajulishe pia umefunga biashara la sivyo hiyo TIN itaendelea kuonekana inafanya hiyo biashara uliyofanyiwa makadirio.
 
Kalipe Deni mkuu na hakikisha umebadili iyo TN vinginevyo bado utasomeka mlipa Kodi! Kumbe adi TN ulibadili huwezi kuwa na TN ya biashara kama hufanyibiashara! Me nilifunga biashara sikubadili TN wakawa wananitumia msg za kwenda kulipa kodi nilivyo ona msg zimezidi nikaenda nikaambiwa nina daiwa nikawapa barua zao na za serekali za mtaa za maombia ya kufunga biashara wakarudisha kumbu kumbu saw a maana nao ata kama wana juwa na wewe huna kumbu kumbu za maandishi watakupiga rushwa au vyovyote vile!
 
Laki inasoma vipi kwenye system wakati hajalipa
Alienda TRA wakampa fomu yenye control number ili akalipe laki 1 baada ya mahojiano mafupi.

Ina maana alifanyiwa makadirio ya kodi. Labda kama alikadiliwa 0.00 Tsh kwa kuwa alienda mwishoni mwa mwaka. Lakini laki 1 inasomeka kwenye system.

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…