Naomba nichukue nafasi hii kuelimisha na kueleza utaratibu kamili wa namna ya kupata TIN ya BIASHARA hapa maana yake kuna TIN si ya Biashara na process nzima ya uanzishwaji wa biashara kwa kujisajili TRA.
1. Utaende ofisi za TRA utapatiwa fomu 3.
A. Fomu kwa ajili ya maombi ya TIN NB TIN UNAWEZA PIA JAZA MWENYEWE ONLINE LKN UTALAZIMIKA KUFIKA TRA KUPATA CHETI HALISI.
B. Fomu kwa ajili ya mwenyekiti wa mtaa au kitongoji ambacho utafanyia biashara yako
C. Fomu kwa ajili ya maelezo yako binafsi ambayo huwa Kurasa 3.
2. Ukishajaza hizo fomu utarudisha TRA sambamba na vitu vifuatavyo.
A. Mkataba wa pango wa sehemu ile ambayo utafanyia bishara yako, hapa kama hujapanga basi utalazimika kupeleka risiti ya kodi ya jengo inayoonesha jina sawa na lako au Barua ya mwenyekiti wa mtaa/kitongoji yenye kuthibitisha kuwa eneo lako sio la kudumu au ni banda la kuhamishikika na hujapanga.
B. Passport size zako 2 hizi ni kwa ajili kufungulia faili hapo TRA.
3. Utaratibu wa makadirio hufata hapa sasa huzingaitia MAUZO na sio MTAJI. NASISITIZA TENA HUZINGATINA MAUZO NA SI MTAJI. Lakini hapa pia unaweza KIJIKADIRIA KODI WEWE MWENYE KWA SHARTI LA KUFILE RETURN ZAKO KILA MWAKA.
4. Ukishakadiriwa kodi na kusaini sasa utatatikiwa kulipa angalau awamu moja + Zile kodi ya zuio na kodi ya stampu kama sehemu yako umepanga.
AFTER HIYO SASA UNARU TRA KUOMBA TAX CLEARANCE.
5. UKIPATA HIKO CHETI SASA NDIO UNAENDA HALMASHAURI KUANZA PROCESS ZA KUPATA LESENI YA BIASHARA.
NAAMINI KWA UCHACHE NIMESAIDIA WENGI NA NIMEELEWEKA.
Sent using
Jamii Forums mobile app