Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Happy kwenye kumkata baba mwenye pango akikataa nachukua hatua zipi?
Ni swali zuri kwn changamoto kubwa ya jambo hili ipo ktk utekelezaji ambapo kisheria anawajibika ni baba mwenye nyumba yako.

Namna ya kumlazimisha mwenye nyumba ni wakati wa kuandikishana mkataba wewe hakikisha na yeye anaandika TIN yake pale ambapo utaupeleka mkataba ule TRA kisha mwbie afisa wa TRA kuwa mwenye nyumba nimemlipa pesa kamili na hataki kukatwa hivyo wao wampigie cm na kumwambia aende ofisi za TRA kisha atapewa elimu na kupewa tozo yake ya kodi ya zuio kwa ushahidi wa mkataba wa pango mlioingia nae.

Kwa kuwa TRA wamempa elimu na kumlazimisha naamini hatasumbua tena akiona umemkata na kumpa risit yake ya malipo ya koi ya zuio
 
Je wajibu wako ulikuwa ni nini?
1. Ulikuwa na haki ya kuhoji kiwango hicho amekipata vipi hadi kukuambia ukalipie

Angalizo: lkn pia wkt wa kuomba TIN kuna vielelezo ambavyo uliambiwa kupeleka. Miongn ni pamoja na mkataba wa pango, picha, barua ya serikali ya mtaa na kujaziwa fomu. Laah, ulienda kama unataka TIN kwa ajili ya kupata leseni ya udreva then ukageuza maelezo ukasema utafanya biashara

2. Je alikuuliza eneo la biashara umepanga? Kama ndiyo alitumia maelezo haya ya kupanga na kufanya 'assumption' kutokana na udogo wa biashara na mauzo kuwa huenda walipa sh 20,000 kwa mwezi.

3. Kama hakukuuliza pia alifanya 'assumption' umepanga. Je kama unafanyia biashara kwako ulistahili kulipa? Jawabu NI HAPANA ila angekuuliza umelipia kodi ya jengo? Ambapo maeneo mengi ni sh 10,000 kwa mwaka
Lakini mbona hakuniomba mkataba wa pango aliniuliza tu ni wap unapofungua na mtaji wako ni sh ngapi
baada ya kumpa vielelezo vyote vya serikali ya mtaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je wajibu wako ulikuwa ni nini?
1. Ulikuwa na haki ya kuhoji kiwango hicho amekipata vipi hadi kukuambia ukalipie

Angalizo: lkn pia wkt wa kuomba TIN kuna vielelezo ambavyo uliambiwa kupeleka. Miongn ni pamoja na mkataba wa pango, picha, barua ya serikali ya mtaa na kujaziwa fomu. Laah, ulienda kama unataka TIN kwa ajili ya kupata leseni ya udreva then ukageuza maelezo ukasema utafanya biashara

2. Je alikuuliza eneo la biashara umepanga? Kama ndiyo alitumia maelezo haya ya kupanga na kufanya 'assumption' kutokana na udogo wa biashara na mauzo kuwa huenda walipa sh 20,000 kwa mwezi.

3. Kama hakukuuliza pia alifanya 'assumption' umepanga. Je kama unafanyia biashara kwako ulistahili kulipa? Jawabu NI HAPANA ila angekuuliza umelipia kodi ya jengo? Ambapo maeneo mengi ni sh 10,000 kwa mwaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi inawezekana kwenda kubadilisha taarifa kama taarifa za mwanzo hukuzitoa kwa usahihi kutokana na kukosa uelewa?
 
Ndiyo uwezekano huo upo ila fuata hatua hizi:
1. Utaandika barua kwa kamishna wa kodi
2. Katika kichwa cha habari usisahau kuandika TIN yako
3. Utatoa maelezo ambayo wewe unaamini ni sahihi na ukiambatanisha vielelezo kama ushahidi wako wa iliyoyaandika ambayo ni ya kweli na sahihi
4. Suala lolote linalohusisha malipo jitahidi yaw na risit ya EFD kwn ndiyo hutambulika rasmi
Hivi inawezekana kwenda kubadilisha taarifa kama taarifa za mwanzo hukuzitoa kwa usahihi kutokana na kukosa uelewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimeelewa kidogo....maana Mimi nikikatwa 14000, ndipo nipate tax clearence, hii ndio itapelekea kutafuta leseni ya biashara ya masuala ya tigo pesa na mpesa.....pia walinikadilia kiasi cha Kodi ninachotakiwa kulipa Kila mwaka......kama laki Mona hivi,wakini wakagawa kwa awamu nne.....swali langu kwanini nilipe Kodi hiyo ya Kila mwaka wakati nimekata leseni??? wajuzi nipeni elimu hapoo
 
nimeelewa kidogo....maana Mimi nilikatwa 14000, ndipo nipate tax clearence, hii ndio nitapelekea kutafuta leseni ya biashara ya masuala ya tigo pesa na mpesa.....pia walinikadilia kiasi cha Kodi ninachotakiwa kulipa Kila mwaka......kama laki Moja hivi,wakini wakagawa kwa awamu nne.....swali langu kwanini nilipe Kodi hiyo ya Kila mwaka wakati nimekata leseni??? wajuzi nipeni elimu hapoo
 
nimeelewa kidogo....maana Mimi nikikatwa 14000, ndipo nipate tax clearence, hii ndio itapelekea kutafuta leseni ya biashara ya masuala ya tigo pesa na mpesa.....pia walinikadilia kiasi cha Kodi ninachotakiwa kulipa Kila mwaka......kama laki Mona hivi,wakini wakagawa kwa awamu nne.....swali langu kwanini nilipe Kodi hiyo ya Kila mwaka wakati nimekata leseni??? wajuzi nipeni elimu hapoo
Mkuu TEMBO WANGU
Nakushauri pitia vizuri kabisa uzi huu hapa chini nauweka utapata majibu mazuri na kukata kiu yako ya kutaka kujua masuala mbalimbali juu ya kodi. Niwie radhi kama nitakuwa nimekukwaza kwa jawabu hili

MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakubwa. Naomba kuuliza ili nipatiwe TIN no na tax clearance TRA kwa ajili ya utaratibu wa leseni ya biashara natakiwa niorodheshe vitu gani na niwe naa gharama gani ili kukamilisha utaratibu huu.

Nimeuliza sababu naimani wapo watu walishawahi kufanya hizi taratibu na ni vyema nifahamu ili nikienda nimeenda kuepusha muda na adha ya kuulizia na kurudi. N.B nataka leseni kwa ajili ya laini ya uwakala. Asanteni sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda ofisi za halmashauri unayotaka kufanya biashara, watakupa fomu ambayo utaipeleka serikali ya mtaa unapotaka kufanyia biashara baada ya hapo utaenda TRA mahali ulipo, utapewa fomu ya maombi ya TIN mpya na TAX CLEARANCE . Mahitaji mengine utakutana nayo kwenye hizo fomu za Halmashauri na TRA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da umeniwahi mi mwenyewe ndo nataka kupata tin namba ya biashara duka la reja reja..ngoja tusubili muogozo.
Wakuu tambueni kuwa mchakato wote wa TRA na hizo fomu za Jiji / Manispaa / Miji ni free ila mtakuja kulipia leseni ( Kila halmashauri ina viwango vyake ) . Kodi ya TRA itategemea na mtaji unaotaka kuanza nao na busara ya ofisa wa TRA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu tambueni kuwa mchakato wote wa TRA na hizo fomu za Jiji / Manispaa / Miji ni free ila mtakuja kulipia leseni ( Kila halmashauri ina viwango vyake ) . Kodi ya TRA itategemea na mtaji unaotaka kuanza nao na busara ya ofisa wa TRA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfano mtaji wa milion 3.hapo mkuu Kwa dsm Kodi yke inakuaje na hio kupata tin number ni mpk uwe na frame tiyari waje waestimate jumla ya bidha au??
 
Nenda ofisi za halmashauri unayotaka kufanya biashara, watakupa fomu ambayo utaipeleka serikali ya mtaa unapotaka kufanyia biashara baada ya hapo utaenda TRA mahali ulipo, utapewa fomu ya maombi ya TIN mpya na TAX CLEARANCE . Mahitaji mengine utakutana nayo kwenye hizo fomu za Halmashauri na TRA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseeeeee maelezo haya mnayatoaga wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu tambueni kuwa mchakato wote wa TRA na hizo fomu za Jiji / Manispaa / Miji ni free ila mtakuja kulipia leseni ( Kila halmashauri ina viwango vyake ) . Kodi ya TRA itategemea na mtaji unaotaka kuanza nao na busara ya ofisa wa TRA

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba nichukue nafasi hii kuelimisha na kueleza utaratibu kamili wa namna ya kupata TIN ya BIASHARA hapa maana yake kuna TIN si ya Biashara na process nzima ya uanzishwaji wa biashara kwa kujisajili TRA.
1. Utaende ofisi za TRA utapatiwa fomu 3.

A. Fomu kwa ajili ya maombi ya TIN NB TIN UNAWEZA PIA JAZA MWENYEWE ONLINE LKN UTALAZIMIKA KUFIKA TRA KUPATA CHETI HALISI.

B. Fomu kwa ajili ya mwenyekiti wa mtaa au kitongoji ambacho utafanyia biashara yako
C. Fomu kwa ajili ya maelezo yako binafsi ambayo huwa Kurasa 3.
2. Ukishajaza hizo fomu utarudisha TRA sambamba na vitu vifuatavyo.

A. Mkataba wa pango wa sehemu ile ambayo utafanyia bishara yako, hapa kama hujapanga basi utalazimika kupeleka risiti ya kodi ya jengo inayoonesha jina sawa na lako au Barua ya mwenyekiti wa mtaa/kitongoji yenye kuthibitisha kuwa eneo lako sio la kudumu au ni banda la kuhamishikika na hujapanga.

B. Passport size zako 2 hizi ni kwa ajili kufungulia faili hapo TRA.
3. Utaratibu wa makadirio hufata hapa sasa huzingaitia MAUZO na sio MTAJI. NASISITIZA TENA HUZINGATINA MAUZO NA SI MTAJI. Lakini hapa pia unaweza KIJIKADIRIA KODI WEWE MWENYE KWA SHARTI LA KUFILE RETURN ZAKO KILA MWAKA.

4. Ukishakadiriwa kodi na kusaini sasa utatatikiwa kulipa angalau awamu moja + Zile kodi ya zuio na kodi ya stampu kama sehemu yako umepanga.
AFTER HIYO SASA UNARUDI TRA KUOMBA TAX CLEARANCE.
5. UKIPATA HIKO CHETI SASA NDIO UNAENDA HALMASHAURI KUANZA PROCESS ZA KUPATA LESENI YA BIASHARA.

NAAMINI KWA UCHACHE NIMESAIDIA WENGI NA NIMEELEWEKA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jinsi ya kupata TIN number unatakiwe uende ofisi ya TRA iliyopo wilayani kwako na vitu vifuatavyo, kitambulisho chako cha taifa, mkataba wa pango uliopanga, kama fremu ni yako mwenyewe basi uende na risiti na ya kodi ya majengo, barua ya serikali ya mtaa uliopanga hiyo fremu,na picha yako moja ya passport size, baada ya kukamilisha hivyo vitu unaenda TRA watakukadiria kodi( kodi ya TRA inatokana na mtaji wako).

Baada ya hapo utapewa TIN number siku hiyo hiyo, baada ya kupewa tin number utatakiwa kulipa kodi waliokwambia, ukishalipa hiyo kodi utarudi TRA ili upewe tax clearance. kama Kuhusu kupata leseni ya biashara, kwa sasa mfumo umebadilika, hakuna haja ya kwenda halmashauri utaomba leseni online na baada ya hapo utapewa control number online utaenda kulipia bank au kwenye simu na leseni yako utaipata baada ya siku chache tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nichukue nafasi hii kuelimisha na kueleza utaratibu kamili wa namna ya kupata TIN ya BIASHARA hapa maana yake kuna TIN si ya Biashara na process nzima ya uanzishwaji wa biashara kwa kujisajili TRA.
1. Utaende ofisi za TRA utapatiwa fomu 3.
A. Fomu kwa ajili ya maombi ya TIN NB TIN UNAWEZA PIA JAZA MWENYEWE ONLINE LKN UTALAZIMIKA KUFIKA TRA KUPATA CHETI HALISI.
B. Fomu kwa ajili ya mwenyekiti wa mtaa au kitongoji ambacho utafanyia biashara yako
C. Fomu kwa ajili ya maelezo yako binafsi ambayo huwa Kurasa 3.
2. Ukishajaza hizo fomu utarudisha TRA sambamba na vitu vifuatavyo.
A. Mkataba wa pango wa sehemu ile ambayo utafanyia bishara yako, hapa kama hujapanga basi utalazimika kupeleka risiti ya kodi ya jengo inayoonesha jina sawa na lako au Barua ya mwenyekiti wa mtaa/kitongoji yenye kuthibitisha kuwa eneo lako sio la kudumu au ni banda la kuhamishikika na hujapanga.
B. Passport size zako 2 hizi ni kwa ajili kufungulia faili hapo TRA.
3. Utaratibu wa makadirio hufata hapa sasa huzingaitia MAUZO na sio MTAJI. NASISITIZA TENA HUZINGATINA MAUZO NA SI MTAJI. Lakini hapa pia unaweza KIJIKADIRIA KODI WEWE MWENYE KWA SHARTI LA KUFILE RETURN ZAKO KILA MWAKA.
4. Ukishakadiriwa kodi na kusaini sasa utatatikiwa kulipa angalau awamu moja + Zile kodi ya zuio na kodi ya stampu kama sehemu yako umepanga.
AFTER HIYO SASA UNARU TRA KUOMBA TAX CLEARANCE.
5. UKIPATA HIKO CHETI SASA NDIO UNAENDA HALMASHAURI KUANZA PROCESS ZA KUPATA LESENI YA BIASHARA.
NAAMINI KWA UCHACHE NIMESAIDIA WENGI NA NIMEELEWEKA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi mkuu, ila kwa sasa leseni unaomba online, nilienda halmashauri ndio nikaambiwa hivyo, na mimi pia niliomba online, link hii hapa Home - TNBP

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom