Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Naomba kuuliza kama una TIN na unataka kujua TRA wanakudai kiasi gani unaweza kujua kupitia WEB yao au mpaka uende ofisini kwao?
 
Katika manada unaoendelea kuna wadau wanaweka Bid Price ambazo hazina uhalisia. Nadhani TRA wangekuwa na Closing Price. Kwa sasa wana Starting Price tu. Angalia hizi picha uone hizo Highest Bid Prices zilizowekwa na wadau🙂🙂.
 
Duh

Wanayo TIN n.k.
Itabidi waulize walioweka hizo bei au wafute
 
Noted, thanks
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tuacheni roho ya kubania. Jana nilishiriki mnada wa magari wa TRA online. Nilikuwa nataka Noah Town Ace. Wanunuzi tulikuwa wanne, muda wa marejuhi akaibuka mmoja eti ame-bid Noah kwa Tshs 57,000,000/= wakati bei elekezi ya TRA ilianzia Tshs 4,500,000/= Mie nilifika mpaka Tshs 5,550,000/= ilikuwa niichukue sema akaibuka huyo "Dr shika" wa mtandaoni kuvurugia tu watu mingo zao. Haya sasa kalipie sasa hiyo 57M kwa Noah used.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona alidhani Landcruiser V8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…