Za majukumu wandugu? Bila shaka Mungu anasaidia
Niliagiza mizigo Ali express order zilikua 6 mwezi Desemba mwaka Jana. Ila kutokana na janga la Corona mizigo ikachelewa na nikajua imepotea sababu ndani ya mwezi tu huwa unapokea ila this time ilivuka muda inaonekana imewaasili lakini sjapewa taarifa na Posta na corona ipo high nikaona nishapoteza.
Tarehe 30 mwezi huu wa Machi ikafika, Posta walinitumia text. Nimeenda Posta wakasema mzigo mmoja upo TRA nenda kaufuate ila hii mingine wameiruhusu chukua.
Nikaenda mpaka TRA sehemu husika incharge nilimkuta jamaa mmoja nikamsalimu nikampa maelezo. Akaniambia ni kweli mzigo upo ila niliuzuia inabidi ulipe kodi kisha uchukue. Ilikua ni mini sewing machine yaani kimashine cha kushonea unashika mkononi. Akaniuliza hii mashine ulinunua bei gani? Nikamwambia Tshs. 5,000 akaguna. Akauliza na zile memory nikamwambia moja Tshs. 4500 so pale zipo 2 jumla Tshs. 9,000.
Akaendelea kuuliza "Zina ukubwa gani?" Nikamwambia GB 16. Akauliza "kwanini usinunue hapa mpaka ununulie China?" Nikamwambia bei ni ndogo, hiyo Tshs. 4,500 Tanzania huwezi kupata memory card ya GB 16, hata GB 2 hupati. Akasema sawa, sasa iyo mashine inabidi ulipe kodi. Nikamuuliza kiasi akasema lipia Tshs. 35,000.
Nikamwambia kitu cha Tshs. 5,000 kodi yake Tshs. 35,000, cha laki si itakua laki 5? Akasema yani iyo ni nje ya mfumo tukiingiza kwenye system hapa inazidi hiyo. Nikamuuliza kodi mnakata asilimia ngapi? Akasema hawezi kusema hadi auone mzigo. Nikamuuliza tena, mfano naagizia kitu cha Tshs. 70,000 kodi ni kiasi gani na inakatwa kwa asilimia ngapi? Akasema dogo mpaka tuone mzigo maana kuna VAT na vitu gani sijui.
Ila nahisi kengele iligonga kichwani make kwamba huyu dogo anaelewa hizi vitu kutokana na maswali yangu. Akaniambia kwahiyo lipia basi nina ishu nyingi za kufanya. Nikamwambia bro sina hela halafu kama ni kodi inabidi nilipe chini ya iyo pesa niliyonunulia nahisi ata elfu moja haifiki.
Akatulia akanicheki then akasema fungua simu yako nicheki hiyo bei, bahati mbaya simu haikuwa na chaji ilikuwa 4% tu. Akanipa charger yake nikafungua Ali Express nikamuonesha akacheki akaona ni sahihi sjadanganya. Akatoa karatasi akaandika realese statement akanipatia kamzigo kangu.
Ila nilipanga asiponipa naenda uongozi wa juu, potela mbali hata kama ni cha 5,000 ni pesa yangu.
Nimejifunza kitu, TRA inachafuka kutokana na watu waliopewa usimamizi kwa tamaa zao. Ukiwa muoga wanakupiga hasa au huo mzigo wako utaacha na hupati kitu. Wajuzi mnisaidie kodi ya vitu kama hivyo ni asilimia ngapi inakatwa ili nitakapoagiza mzigo mkubwa nijue kabisa naenda lipa kodi kiasi gani maana yule jamaa alishindwa kuniambia ukweli.
Sijawahi kutana na TRA Posta ila sasa ndio wameanza kukagua na wanafungua ndani wanacheki kuna nini japo sijajua mikoa mingine ipoje na kama haipo basi jiandaeni mi nipo mkoani.
.