Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

mnadanganyana

kwanza kodi sio VAT peke yake

pili thamani ya kitu sio bei uliyonunulia

ndio maana hata ukipewa bure bado utalipishwa kwa vile thamani yakr sio sifuri kwa sababu eti umepewa bure

tena ukipewa bure au kwa bei ya kutupa ndio utalimwa excise duty ya kutupa takataka, au dumping fee, maana Afrika haitaki kuwa tabata dampo la dunia

thamani ya kitu hapa Tanzania inapangwa na TRA

hicho kiji mashine TRA waliona wasipoteze muda kukithaminisha maana hakina demand, hakijulikani, hakitumiwi hapa nchini, wakakupetesha

lete mashine la kushoma magunia uone kama watacheki thamani yake kwenye simu yako...
Fact

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hilo subaru wakati linauzwa halilipiwi kodi, Kwanini mnapiga thamani ya kuuzwa ikiwa bado halijauzwa na likiuzwa kunakuwa
na kodi tena.
Likishaingia nchini linaitwa gari la mkononi, industry parlance at Lumumba and Kidongo Chekundu.

By law of the land, gari la mkononi likiuzwa hakuna sales tax, au VAT. Kuna nominal one percent, call it documentation fee if you will. Milioni tano mauzo ya gari TRA wanapata 50,000.

Ndo maana wanaikata ushuru inapoingia.

Na thamani ya Subaru is written on stones. Uzunguni umeipata bure, good for you. Nimeweka kikokotoo cha TRA kinachoonyesha hawataki kujua umeipata pataje. They couldn't care less.

Huwezi kuwaonyesha bill of lading kwenye simu yako eti ndio proof of purchase. They will dress you down, watakuitia kitoto kimetoka tax school juzi kitakwambia "Mzee ngoja tukuelimishe." Very embarassing, very mortifying.
 
Wadau, ushauri wenu ni muhimu sana hapa kwa mustakabali wa maisha yangu na familia yangu.

Moja kwa moja kwenye mada.

Ipo hivi, mimi nina kampuni ambayo kwa sasa sitaitaja kwa sababu suala bado haijaisha, mwaka 2018 nilienda TRA kufahamu taratibu juu ya ulipaji wa kodi za serikali. Walinikabidhi kwa wakala wao wa mahesabu (tax consultant) kwa kuwa kipindi hicho sikuwa na mhasibu. Wakala huyu alianza kutengeneza hesabu za miaka miwili 2017 na 2018, baada ya kukamilisha hesabu za miaka hiyo miwili alonionyesha kiwango cha kodi nachotakiwa kulipa kilikuwa jumla ni millioni 5.8, hivyo nilisaini mahesabu Yale na akayapeleka TRA.

Sikujua kama TRA watapitia tena mahesabu yale kama taratibu zao zinavyowataka wanaita assessment, hivyo baada ya kuyapitia walisema ninatakiwa kulipa kodi ya Tshs millioni 45.3, kwa kweli nilishangaa sana hivyo niliamua kuwaona ili nijue tofauti kubwa kiasi imesababishwa na nini. Walinitaka niende na tax consultant wangu ili watupe maelezo, lakini cha ajabu huyu tax consultant alikataa kwenda TRA na kwa ujumla hakuonyesha ushirikiano kabisa juu ya hili suala, na mimi sina uweledi wowote wa masuala ya kihasibu.

Niliamua kuwaandika barua TRA kuwajulisha kuwa hayo mahesabu siyatambui na nahitaji muda zaidi niyapitie na wakala mwingine wa TRA (tax consultant) mwingine ambaye nilimchagua mwenyewe. Cha ajabu TRA walinikatalia ombi langu na kumtaka tax consultant wa awali arekebishe hizo hesabu, tulipewa muda kama wiki moja.

Alipomaliza kurekebisha na kuzirudisha tena TRA ili ziendane na mahesabu ya awali, ilishindikana na nilitakiwa kulipa kodi ileile ya 45.3 million, pia wamenipa mwezi mmoja niwe nimeshalipa la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.

Kwa kifupi, kampuni ninayoiongoza ni mpya na haijawahi kuwa hata na Tshs 5 millioni bank, hivyo kwa ujumla hivyo kodi haiwezi kulipika. Wamesema kama sikubaliani na hivyo kodi inabidi nikate rufaa kwa kamishna wa TRA kwa sharti la kulipa theruthi ya kodi ninayodaiwa ambayo ni Tshs 15.1 millioni, ambazo pia hazilipiki maana kampuni haina uwezo wa kulipa ili rufaa isikilizwe, hata hivyo nimekosa imani kabisa na hawa TRA kwa sababu hata hivyo rufaa nikikata sina imani kama nitafanikiwa.

Nauliza hivi: Haiwezekani nikafungua kesi kwenye mahakama zetu za kawaida kuomba hesabu zirudiwe upya na kusitisha utekelezaji wowote kutoka TRA? Au ni njia gani nzuri naweza kutumia ili nijiepushe na hili janga?

Naombeni ushauri wenu kwa wale waliopitia suala kama langu au wale wanaofahamu wanishauri nini nifanye, naomba samahani kwa makala ndefu, japo nimejitahidi kuifupisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bigmash,

Pole ndungu. Nakushauri omba appointment na waziri mwenye Dhamana. Kuna miwatu pale TRA ni mijizi hatari badala kuinua Wajasiliamali wadogo kazi yao kuwapoteza hadi Inasababisha Yeboyebo za mezani wanauza Wachina.

Naamini asilimia100 utafanikiwa ukimuona Waziri husika. Kama ni ngumu sana kumuona mvizie majumba ya Ibada au mikutano ya kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani nilisikia Ndugu Imani Madega ni mwanasheria anaye husika na kesi za kibiashara.
Kama unaweza mtafute huyu mdau ndugu yake Ridhiwani JK.

Nenda ukapate ushauri wa kisheria haraka sana. Nahisi harufu ya rushwa katika hili sakata.
Unatengenezewa mazingira uombe kufanyiwa wepesi kwa kuwapa chochote kitu cha kutunisha matumbo ya wadau fulani hapo Forodhani.
 
bigmash,

Pole ndungu. Nakushauri omba appointment na waziri mwenye Dhamana. Kuna miwatu pale TRA ni mijizi hatari badala kuinua Wajasiliamali wadogo kazi yao kuwapoteza hadi Inasababisha Yeboyebo za mezani wanauza Wachina. Naamini asilmia100 utafanikiwa ukimuona Waziri husika. Kama ni ngumu sana kumuona mvizie majumba ya Ibada au mikutano ya kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa, japo nipo mkoani lakini nitajaribu kabla muda walionipa haujaisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani nilisikia Ndugu Imani Madega ni mwanasheria anaye husika na kesi za kibiashara.
Kama unaweza mtafute huyu mdau ndugu yake Ridhiwani JK.

Nenda ukapate ushauri wa kisheria haraka sana. Nahisi harufu ya rushwa katika hili sakata.
Unatengenezewa mazingira uombe kufanyiwa wepesi kwa kuwapa chochote kitu cha kutunisha matumbo ya wadau fulani hapo Forodhani.
Nimekusoma mkuu, asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole ndg yangu. Fanya yafuatayo:

Mtafute wakili mzuri akushauri nini cha kufanya.

Pili, usijaribu kukata rufaa kwa hayo majizi ya TRA maana watakupotezea muda tu.

Tatu, hakikisha una copy ya mahesabu ya awali ya hiyo mil 5 uliyoisain ili uwe ushahidi kokote utakapohitajika au hata mahakamani.

Mwisho, usidhubutu kulipa kulipa kiwango chochote kile kilichoongezeka nje ya assessment ya awali. Hao wahuni wa TRA sio mwisho wa suluhu wa jambo hili. Ni mijitu tu yenye roho mbaya lakini ukweli sio msimamo wa Serikali hii.

Ikikupendeza ni PM nikupe some abc on how to go about this... bigmash,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole ndg yangu. Fanya yafuatayo:

Mtafute wakili mzuri akushauri nini cha kufanya.

Pili, usijaribu kukata rufaa kwa hayo majizi ya TRA maana watakupotezea muda tu.

Tatu, hakikisha una copy ya mahesabu ya awali ya hiyo mil 5 uliyoisain ili uwe ushahidi kokote utakapohitajika au hata mahakamani.

Mwisho, usidhubutu kulipa kulipa kiwango chochote kile kilichoongezeka nje ya assessment ya awali. Hao wahuni wa TRA sio mwisho wa suluhu wa jambo hili. Ni mijitu tu yenye roho mbaya lakini ukweli sio msimamo wa Serikali hii.

Ikikupendeza ni PM nikupe some abc on how to go about this...

Sent using Jamii Forums mobile app
I like it mkuu

WANA JAMII FORUMS, TUSIFANYE MAKOSA TENA OCT 2020
 
Back
Top Bottom