Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Nijuavyo mimi, unaandika barua kwa kamishna general kuomba mapitio mapya ya assessments ya makadirio yako, muda huo huo unatakiwa kuwa umelipa theluth moja ya ulichokadiriwa then mkishindwana ndio mnapelekana Kwenye court of arbitration.
 
Kuna rafiki yangu mmoja alifunga kampuni yake akarudi kwao Kenya kwa sababu ya TRA. Sijui kama walipata faida gani baada ya jamaa kufunga.

Walikuwa wanatengeneza mazingira ya rushwa.

Kwa hio mtaalamu hapo hao wajinga wanatengeneza mazingira ya rushwa.
Usiwape hata senti huo ni uonevu.

Wewe nenda kwa waziri au Mkurugenzi wa TRA
 
Wanataka kukuibia hao taarifa za mwanzo ndiyo sahihi hizo za sasa ni wizi wa kiwango cha lami,

Adui wa mwafrika ni mwafrika mwenzake yaani umejitahidi umeanzisha kampuni halafu wanatokea makuda kukurudisha nyuma kirahisi kiukweli imeniuma Sana
 
nijuavyo mimi,unaandika barua kwa kamishna general kuomba mapitio mapya ya assessments ya makadirio yako,muda huo huo unatakiwa kuwa umelipa theluth moja ya ulichokadiriwa then mkishindwana ndio mnapelekana Kwenye court of arbitration.
Hilo walinieleza, tatizo hata hiyo theluthi ninayotakiwa kulipa ili suala langu lisikilizwe kwa kamishna sina, maana ni 15.1 million, ni parefu sana kwangu ndugu yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisikia laana ndiyo hii. Yaani mwenzako anataka kwenda mbele wewe unamrudisha nyuma. Tutafika kweli?
Ninakulilia nchi yangu Tanzania. Mtu unakuaje na moyo mbaya kiasi hicho. Ndiyo maana saa nyingine tunapukutika tu kwa ajali na magonjwa mengine kwa ajili ya maovu yetu na hakuna jinsi.Hata nafsi yako haikuhukumu kwa maovu unayomfanyia mwenzako.
 
Hilo walinieleza, tatizo hata hiyo theluthi ninayotakiwa kulipa ili suala langu lisikilizwe kwa kamishna sina, maana ni 15.1 million, ni parefu sana kwangu ndugu yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa inaonekana wanataka rushwa. Baada ya kusikiliza kile kisa cha mfanyabiashara wa Kariakoo aliyeharibiwa mali zake na TRA na rais kuamuru alipwe halafu wakawa wanamzungusha na kutaka kumuua nimegundua TRA wafanyakazi wengi ni wezi. Hakuna cha kodi wala nini wanachotaka ni rushwa. I wish rais avunje TRA na waliopo waondolewa wote na kuanza kuundwa mpya yenye wafanyakazi wapya. Wakikuletea ujinga fanya taratibu z kampuni kuwa mufilisi. Ukitaka kuanzisha nyingine kuna mbinu nyingi tu za kufanya. Na mbaya zaidi hata ukienda kwa mawakili nao unaweza kukuta unaingia gharama ambayo huwezi kuilipa. Plole sana ndugu yangu.
 
Duh....! Lakini hakikisha wewe na kampuni yako unakuwa na mwanasheria! Usingesumbuka namna hii! Usikate tamaa..ikiwezekana fika level ya juu
 
Mimi pia kampuni yangu ilianza hivi karibuni na mshauri wa kodi alinipigia hesabu ya laki 2 na 10 maana sikuwa nimeanza kuingiza kitu bado ila akanishauri nianze kulipa hiyo

TRA wameniletea 12.9 M sasanikawaambia waje ofisini maana ofisi ina laptop, modem, kiti, kimeza cha kufix ukutani, extension na feni

Ilibidi nicheke, wakaniambia nitud kwa mtaalamu wa hesabu kurekebisha, mtaalamu anataka laki 6 kurekebisha nikasema nyie wote mafala.

Nikaandika barua ya kukana hesabu zao, hawajajibu hadi leo na nimesha funga ofisi nafanya mchakato wa kufunga kampuni nijikite ktk biashara haramu.

Sent using COVID-19
 
Mimi ndo maana kulipa kodi huwa napiga chenga
 
Nali, Mungu akuongoze uweze kumsaidia, huna napatwa na hasira sana ninapoona watu waovu kama hao wa TRA wanachotaka kumfanyia huyo jamaa.

Watu hawana kabisa Uadilifu
 
Sijuti, nikiona story kama hizi napata hasira sana, halafu unakuta mtu amekaa na mke wake na watoto wanafurahi wakati huku kashamuumiza mtu mwengine na kumrudisha nyuma. Watu wa aina hii ndo wa kupewa kesi ya uhujumu uchumi
 
Washawishi hayo MAJIZI/MAJAMBAZI wa TRA uwape 10 millions ili yaishe kisha nenda PCCB ukawakamatishe, usiwe mnyonge ndugu yangu hii dunia imejaa mbwa kama hao wanaofurahia kuona wenzao hawapigi hatua!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusichojua watu wengi tunafungua kampuni bila kujua sheria za kampuni na mambo ya kodi kuhusu kampuni, hesabu zawezakua za kawaida tu lkn kwa kua miaka mi2 hujapeleka return na wala hesabu hujafanya hesabu zinabadilika pakubwa sana, inawezekana wapo sawa kisheria sema hujataka kukaa nao wakakuelewesha vizuri ukaelewa, hesabu zako zinaeza kua sahihi lkn penati zikakucost kutokana na sheria za kampuni mfano mtu binafsi usipofanya makadirio tu kwa mwaka faini yake karibu laki 7, sasa wewe miaka mi2 hujafanya makadirio, hesabu wala return hujapeleka, pengine na mashine ya EFD huna unategemea nini?

Sa nyingine hesabu yako sio kubwa hivyo lkn makosa yako yanatoa mwanya wa kukunyanyasa na kutaka rushwa,
Kampuni lazima iwe na mwandaa hesabu ambae hulipwa sio chini ya laki 5 adi ml1 naa, na mhakiki wa hesabu pia nae analipwa.

Kabla kufungua kampuni msome sheria za kodi kwanza badala ya kusoma za brela pekee, kampuni ina mambo mengi sanaa sio km biashara ya mtu binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakushauri malalamiko yako yapeleke TRAT au TRAB utapata msaada koz hizo ndo tribunal mkishindana sasa hapo unaweza ku appeal kwenye high Court au Court of appeals

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda twitter pale utawakuta andika kisha uwatag ili hili suala lijadilowe nationalwide. La sivyo ndugu, utapoteza.
 
Back
Top Bottom