Niliomba kwenda taasisi nyingine , nikaambiwa niandike barua ila mwajiri lazima aipitishe na ikifika kwao wao watamaliza kila kitu hadi utumishi baada ya mwajiri wangu kupitisha, nilipoandika kwa mwajiri, ali-comment kuwa "asiondoke na akiondoka anaomba afanyiwe replacement" hivyo ilipofika makao makuu dar wakasema hawawezi kuruhusu kwa comment hiyo, njia nyingine waliyotoa ni hiyo ya kubadilishana. Huku kwenye idara za mahakama unapoomba uhamisho, barua inapita sehemu mbili, kwanza kwenye kituo unachofanyia kazi (mahakama za kanda) halafu inaenda makao makuu ya mahakama jijini dar es salaam, kwa hiyo huku barua ilitoka na hiyo comment na ilipofika dar nikaona kimya, kuuliza ndio wakanipa majibu hayo na arternative ya kufanya.