Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Huu Wimbo nakumbuka hivi vipande vipande

(Neno la Mungu lilimjia Yona)×2
Uende Ninawi ukawaambie watu wangu,
Uovu wao umefika mbele zangu..

Yona akapanda merikebu, inayokwenda Tarshishi
Ajiepushe na uso wa Mungu....

Mungu katuma upepo mkali baharini, merikebu ikawa karibu kuvunjika........


Naye Mungu alisikia maombi yake
Nayo samaki na ikamtapika...
 
Kuna mwimbaji alikua anaitwa rose na Salome kati yao kuna alieimba wimbo wa Yule mwizi msalabani alimwambia bwana Yesu ukirudi ktk ufalme wako wa mbingu unakumbuka


Salome akaimba tena watakapokulaza chini na kusema ee bwana bwana mtu huyu tunamjua alikua mwalimu mwema je hayo matendo yako yatakua mema kwa Mungu ili ukipate kibali cha kukufikisha mbinguni
Salome alikua mwimbaji wa Kenya,aliimba pia nyimbo kama,kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe, wachawi wa misri,Na wimbo fulani hivi wa ki lugha kama kijaruo..
 
Naombeni wimbo wenye mashairi haya. .'nakuomba baba baba babaaa uuuunipe mtoto mtotoo '...
 
Kuna mwimbaji alikua anaitwa rose na Salome kati yao kuna alieimba wimbo wa Yule mwizi msalabani alimwambia bwana Yesu ukirudi ktk ufalme wako wa mbingu unakumbuka


Salome akaimba tena watakapokulaza chini na kusema ee bwana bwana mtu huyu tunamjua alikua mwalimu mwema je hayo matendo yako yatakua mema kwa Mungu ili ukipate kibali cha kukufikisha mbinguni
yule mwizi msalabani
Alimwambia Bwana Yesu
Ukirudi katika ufalme
Wako wa mbingu unikumbuke
Unikumbuke pia na mimi
Eeh Bwana Yesu unikumbuke

Yesu wangu unikumbuke Ukirudi kuwachukua
Watoto Wako wateule, kuishi nao juu mbinguni

Ahsante umenikumbusha mbaliiii
 
Kama naweza kuzipata hizi
# hapana rafiki kama yesu by mwakitalu
[HASHTAG]#Martin[/HASHTAG] Gondwe
-Neno lake mungu
-Siku ya kufa kwangu
-Sodoma na Gomora
[HASHTAG]#Gwinamila[/HASHTAG]
 
Pia kulikuwa na wimbo ukiitwa "Sikiliza Wapendwa" uliimbwa na kwaya moja nadhani ya Tabora kwenye early 1980s. Ulikuwa na maneno haya:
"Sikiliza (wapendwa, wapendwa), Niwambie, Bwana Yesu (kateswa, kateswa) msalabani....ni huzuni (sana, sana, sana), ni huzuni....."
 
Kama naweza kuzipata hizi
# hapana rafiki kama yesu by mwakitalu
[HASHTAG]#Martin[/HASHTAG] Gondwe
-Neno lake mungu
-Siku ya kufa kwangu
-Sodoma na Gomora
[HASHTAG]#Gwinamila[/HASHTAG]
Uwiii ahsante

1. Siku ya kufa kwangu, mimi siifahamu
Inanibidi sasa, niyatengeneze maisha....

Mwili wangu ukiwekwa mle kaburini
Ndugu zangu watakuwa wameuzunguka
Kuuaga mara ya mwisho, hapa duniani
Itakuwa huzuni kubwa hapa duniani

Yatengeneze maisha siku ya mwisho. ..
Ukizitubu dhambi, siku ya mwisho utaokoka

Nahisi tu utakuwa unaufahamu huu wimbo

Nilianza safari, kutafuta amani
Lakini dunia yote ni vilio tupu. ..

Mimi nipo Kwa Yesu sitaki mwingine
Sababu dunia yote ni vilio tupu
Nawe mwanadamu mshike Muumba wako
Maana ni Mungu pekee atakusaidia
 
Mojawapo ya nyimbo zilizotulia za Jangalason.

Najua huyu ni mwimbaji machachari anayeimba kwa mtindo wa comedy na nimekuwa nikifuatilia nyimbo zake tokea alipotoa cassette yake ya kwanza ya USIWE KAMA POPO. Ila pamoja na comedy katika kila album huweka japo wimbo mmoja uliotulia usio wa comedy. na huu Niumbie Moyo safi ni mojawapo ya nyimbo zilizotulia toka kwake.

 
Umeuliza kuhusu Sedekia na RHM, ni kwamba Sedekia alishaimba na New Life Band, kama unawajua hawa vijana na band yao.

Ila Tanzania nzima walikuwa wanarekodi RHM.

Sidhani kama itatokea tena Gospel band kama NLB Tanzania

Na sio Sedekia tu ila pia kuna Upendo Kilahiro na Beatrice Muhone.

NLB Walitunga mapambio kama:-

- Iende mbelee injili hiyoo...iende mbeleee

- Ainuliwe Mungu wetu leooo...ainuliwe bwana wa mabwana

- Mji ulee una meremeta umepambwa mauaaa

Unakumbuka?

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
heeeee wewe.... duh. Unao huh wimbo?
Mji ule unameremeta umepambwa maua. Halafu wameimba na ule mwimbo "Sasa nimetambua ya kwamba kwa Yesu kuna raha"..
 
The best ever
.hii ndio kwaya ambayo ilifanikiwa kutunga nyimbo nzuri kwa asilimia 99%

Umenikumbusha mbali sana
Kuna nyimbo ya Goliath alijifanya tishioo dhidi ya taifa la wana Israel,
Wafilisti walipoona shujaa wao amekufa walikimbia mbio wapate kujiponya nafsi zao
 
Kama kuna mtu ana nyimbo zifuatazo anisaidie
"ohooo lulu iko mbinguni"
"katika viumbe vyote vilivyoumba binadamu kaumbika kuliko vyote"
"malebo kakataa kuokoka"

Sikumbuki majina ya walioimba ni akina nani, kichwa changu memory yake ndogo ni 2GB na kimejaa kwa sasa, mnisamehe
Ukisema kichwa chako kina 2gb ya memory unamkufuru Mungu mkuu.
 
Back
Top Bottom