Fredrick Mosenya
Member
- Jul 4, 2016
- 15
- 13
MUNGU akubariki sana umenikumbusha sana,
kaka kuna wimbo ka jin animeusahau ila nakumbuka baadhi ya mameno yake tu"alipofika karibu aliuona mji akaulilia akisema watu wa yerusalemu"Wakuu,
Ninawiwa Kuhuanzisha Uzi Huu Ili Kuwaleta Karibu Wapenzi wa Nyimbo Za Injili za Zamani!
From the 80s,90s and the Early 2000s!
Kuanzia Barabara 13,Aict Shinyanga,Kijitonyama Upendo Group,Na N.k!
Naoma Tubadlshane Audios,Videos na Picha Waimbaji wa Zamani!
Old is Gold!
Fahari ya vijana, ni ..........
Fahari ya wazee, ni kichwa chenye mvi
Fahari ya moyo wangu, ni kuyatenda mapenzi yake Mungu
Sauli Sauli mbona waniudhi
Sauli wawatesa watu wangu
Bwana kachukizwa sana, kamwambia Sauli
Mimi ndimi Yesu unayeniudhi
Ole wako wewe, unayemuudhi
Bwana Mungu wako utahukumiwa
Uwiii ahsante
1. Siku ya kufa kwangu, mimi siifahamu
Inanibidi sasa, niyatengeneze maisha....
Mwili wangu ukiwekwa mle kaburini
Ndugu zangu watakuwa wameuzunguka
Kuuaga mara ya mwisho, hapa duniani
Itakuwa huzuni kubwa hapa duniani
Yatengeneze maisha siku ya mwisho. ..
Ukizitubu dhambi, siku ya mwisho utaokoka
Nahisi tu utakuwa unaufahamu huu wimbo
Nilianza safari, kutafuta amani
Lakini dunia yote ni vilio tupu. ..
Mimi nipo Kwa Yesu sitaki mwingine
Sababu dunia yote ni vilio tupu
Nawe mwanadamu mshike Muumba wako
Maana ni Mungu pekee atakusaidia
Huu Wimbo nakumbuka hivi vipande vipande
(Neno la Mungu lilimjia Yona)×2
Uende Ninawi ukawaambie watu wangu,
Uovu wao umefika mbele zangu..
Yona akapanda merikebu, inayokwenda Tarshishi
Ajiepushe na uso wa Mungu....
Mungu katuma upepo mkali baharini, merikebu ikawa karibu kuvunjika........
Naye Mungu alisikia maombi yake
Nayo samaki na ikamtapika...
yule mwizi msalabani
Alimwambia Bwana Yesu
Ukirudi katika ufalme
Wako wa mbingu unikumbuke
Unikumbuke pia na mimi
Eeh Bwana Yesu unikumbuke
Yesu wangu unikumbuke Ukirudi kuwachukua
Watoto Wako wateule, kuishi nao juu mbinguni
Ahsante umenikumbusha mbaliiii
"Kwa nini wataka kujiua wewe
Inavyoonesha, umeshakata tamaa. ..
Sikumbuki unavyoendelea wala waimbaji mwee
Naupenda mnoooo
1. Safari yao Wana Israel kutoka Misri kwenda Kanani,
Yafanana na safari yetu tuliyonayo kwenda mbinguni,
Tazama wengi hawakuweza kufika kwa sababu walivunja maagizo ya Mungu
2. Mahangaiko na Mahangaiko
Na shughuli za kila siku
Zimewafanya wanadamu, wamsahau Mungu wao
Haha old is gold
Kuna wimbo najitahidi kuukumbuka hapa, unanigomea. Nakumbuka tu sehemu hii kidogo, ni story ya mwanamke Msamaria
"Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia
Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwa Msamaria
Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria"
Nimebarikiwa mnoo...Mke mwema nani atayemuona
Maana ni mali adimu, Mke mwema yu wapi
Ndoa zavunjika, watoto wahangaika
Kisa baba kamuacha mama, eti Mke si mwema.....
Anza darasa upya,
Mkeo huyo baba, ni mke mwema
Ringa, uringe naye
Mkeo huyo ni mke mwema ringa naye,
Mke ni mwili wako, ni nani wewe wachukia mwili wako
Hii mingine miwili
1. Parapanda ya Bwana italia siku ile
Atakaporudi Yesu kuchukua kanisa lake
Tujitayarisheni, siku hiyo ya kutisha
Ole kwa wale wote, wasiomuamini Yesu
Ndipo Bwana atasema ondokeni kwangu,
Ninyi nyote mliolaaniwa na Baba yenu,
Wataomboleza na kusaga meno, watakapotupwa kwenye moto wa milele....
2. Unafikiria nini, ulimwengu ni wa shida
Tena unajidanganya wewe, na mambo ya ulimwengu
Kanisani umeacha ulikuwa unategemewa. ...............
Siukumbuki vizuri uuuh
Mpanzi alitoka kwenda panda mbegu njema shambani mwake
Na zingineee, zilianguka njiani
Na zingineee tena, zilianguka kwenye miiba
Na zingine tena, zilianguka pakavu
Na zingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikazaa moja Mia sitini moja thelathini
Kuna mwingine pia, naibia ibia tu.
Hata baada ya siku sita mwokozi Yesu,
Alipanda mlimani na wanafunzi wake........
Sauti iii, Sauti iii
Sauti iii, Sauti ikatoka
Huyu ni mwanangu mpendwa msikilizeni, atakayowafundisha nayashikeni
Japo melody na sauti siisikii ila hakika maneno Haya yamenibariki.Sijui wametajwa hawa, Bethel Choir walioimba
Wahurumieni
Mungu yu mwema
Sio sisi
Umepoteza Dira
Basi nasema (tunda la roho) etc
Kwa kweli Leo nimebarikiwa mnooo! !!Nimebarikiwa mnoo...
Japo melody na sauti siisikii ila hakika maneno Haya yamenibariki.
Thanks Dada mtumishi HS
Pamoja Mkuu!MUNGU akubariki sana umenikumbusha sana,
Nakuangalizia,uwe na subira!kaka kuna wimbo ka jin animeusahau ila nakumbuka baadhi ya mameno yake tu"alipofika karibu aliuona mji akaulilia akisema watu wa yerusalemu"
Naukumbuka Huo Wimbo,uwe na subira!Sauli Sauli mbona waniudhi
Sauli wawatesa watu wangu
Bwana kachukizwa sana, kamwambia Sauli
Mimi ndimi Yesu unayeniudhi
Ole wako wewe, unayemuudhi
Bwana Mungu wako utahukumiwa
Just a sec!Fahari ya vijana, ni ..........
Fahari ya wazee, ni kichwa chenye mvi
Fahari ya moyo wangu, ni kuyatenda mapenzi yake Mungu
Asante Mkuu kwa Kuchangia Nasi ktk Uzi Huu!Ulyankulu mkubwa mmoja
Asante Mkuu!Ulyankulu mkubwa mmoja
Nafikiri unaitwa hivyo hivyo "Naloli NaloliWadau kuna nyimbo ya kinyakyusa inapigwagwa kwenye masherehe sana. inaimbwa 'Naloli Naloli' anayeijua anisaidie jina lake
Nilinunuaga album zao zote 3 ambazo ziko katika video (ULYANKULU). Nilikuwa nawapenda sana hawa, pamoja na wale akina mama "Wa kwa Mungu hakuna mzee" kutoka Shinyanga ... Hawa wa mama walikuwa wana sauti tamu sana.
Nakumbuka Album hizi na nyimbo zake. Ninazo LAKINI nitawawekea majina ya nyimbo ili iwarahisishie kutafuta.
1. KATIKA VIUMBE VYOTE.
-Katika viumbe vyote
-Palikuwa na mtu (Ayubu)
-Bwana ndiye mchungaji wangu
-Neno la Mungu lililomjia Yona
-Wakati ule wa Nuhu
-Vijana tuamke sote
-Alipofika karibu aliuona mji
-Yesu alipokuwa ameketi.
2. MWENYE MAMLAKA (Mapigano)
-Mwenye mamlaka
-Wakati huo
-Yesu katazama
-Wokovu ni lazima
- Fahari ya vijana
-Safari ya wana wa Israeli
-Ombeni nanyi mtapewa (Paulo & Sila)
-Amri mpya nawapeni (upendo)
-Goliathi
-Kama ndugu yako akikosa
-Sisi ni barua
3. SAMSON & DELILA
-Dunia ya shida
-Samson
-Ufunuo wa Yohana
-Nitamwona Yesu
-Basi nasema
-Yusufu
-Nikifikiria
-Kifo cha Yesu
-Ulimkimbilia Mungu
Kuna hawa nao walikuja juu miaka ya 2000 mwanzoni wanaitwa "THE GOSPEL SOUND SINGERS," kutoka EAGT Singida. Album yao ilibamba sana.
Iliitwa "KILA GOTI LITAPIGWA."
Ilikuwa na nyimbo hizi;
-Wathamani
-Dunia hii
-Kabla sijaokoka
-Yesu tusaidie
-Amechukua masikito yetu
-Mwanzo na mwisho
-Mimi najivunia
-Bwana Yesu
Nk...
Dah! Those days!
Mkuu,nashukuru!ila waweza tuwekea hizo hapa jf?Yesu kawaambia
Na kama ndugu yako akikosa muonye
Akitubu msamehe
Kuliko kumkosesha mmoja wapo,
Wa wadogo hawa
bado,ila waweza lianzisha na ukatuunga!Wadau waliopendekeza group la whatssapp imeundwa?