Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Wakuu,
Ninawiwa Kuhuanzisha Uzi Huu Ili Kuwaleta Karibu Wapenzi wa Nyimbo Za Injili za Zamani!
From the 80s,90s and the Early 2000s!
Kuanzia Barabara 13,Aict Shinyanga,Kijitonyama Upendo Group,Na N.k!
Naoma Tubadlshane Audios,Videos na Picha Waimbaji wa Zamani!
Old is Gold!
kaka kuna wimbo ka jin animeusahau ila nakumbuka baadhi ya mameno yake tu"alipofika karibu aliuona mji akaulilia akisema watu wa yerusalemu"
 
Nimebalikiwa sana na uzi huu, big up sana uliyeanzisha uzi huu,
kuna wimbo mmoja wa zamani nadhani uliimbwa na Wakenya kama sikosei, nakumbuka title ya wimbo ilikuwa "umejivalia ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu" kama kuna mtu anao naomba atupie hapa.
 
Fahari ya vijana, ni ..........
Fahari ya wazee, ni kichwa chenye mvi
Fahari ya moyo wangu, ni kuyatenda mapenzi yake Mungu

Sauli Sauli mbona waniudhi
Sauli wawatesa watu wangu

Bwana kachukizwa sana, kamwambia Sauli
Mimi ndimi Yesu unayeniudhi
Ole wako wewe, unayemuudhi
Bwana Mungu wako utahukumiwa

Uwiii ahsante

1. Siku ya kufa kwangu, mimi siifahamu
Inanibidi sasa, niyatengeneze maisha....

Mwili wangu ukiwekwa mle kaburini
Ndugu zangu watakuwa wameuzunguka
Kuuaga mara ya mwisho, hapa duniani
Itakuwa huzuni kubwa hapa duniani

Yatengeneze maisha siku ya mwisho. ..
Ukizitubu dhambi, siku ya mwisho utaokoka

Nahisi tu utakuwa unaufahamu huu wimbo

Nilianza safari, kutafuta amani
Lakini dunia yote ni vilio tupu. ..

Mimi nipo Kwa Yesu sitaki mwingine
Sababu dunia yote ni vilio tupu
Nawe mwanadamu mshike Muumba wako
Maana ni Mungu pekee atakusaidia

Huu Wimbo nakumbuka hivi vipande vipande

(Neno la Mungu lilimjia Yona)×2
Uende Ninawi ukawaambie watu wangu,
Uovu wao umefika mbele zangu..

Yona akapanda merikebu, inayokwenda Tarshishi
Ajiepushe na uso wa Mungu....

Mungu katuma upepo mkali baharini, merikebu ikawa karibu kuvunjika........


Naye Mungu alisikia maombi yake
Nayo samaki na ikamtapika...

yule mwizi msalabani
Alimwambia Bwana Yesu
Ukirudi katika ufalme
Wako wa mbingu unikumbuke
Unikumbuke pia na mimi
Eeh Bwana Yesu unikumbuke

Yesu wangu unikumbuke Ukirudi kuwachukua
Watoto Wako wateule, kuishi nao juu mbinguni

Ahsante umenikumbusha mbaliiii

"Kwa nini wataka kujiua wewe
Inavyoonesha, umeshakata tamaa. ..

Sikumbuki unavyoendelea wala waimbaji mwee

Naupenda mnoooo

1. Safari yao Wana Israel kutoka Misri kwenda Kanani,
Yafanana na safari yetu tuliyonayo kwenda mbinguni,
Tazama wengi hawakuweza kufika kwa sababu walivunja maagizo ya Mungu



2. Mahangaiko na Mahangaiko
Na shughuli za kila siku
Zimewafanya wanadamu, wamsahau Mungu wao

Haha old is gold

Kuna wimbo najitahidi kuukumbuka hapa, unanigomea. Nakumbuka tu sehemu hii kidogo, ni story ya mwanamke Msamaria

"Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia
Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwa Msamaria
Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria"

Mke mwema nani atayemuona
Maana ni mali adimu, Mke mwema yu wapi
Ndoa zavunjika, watoto wahangaika
Kisa baba kamuacha mama, eti Mke si mwema.....


Anza darasa upya,
Mkeo huyo baba, ni mke mwema
Ringa, uringe naye
Mkeo huyo ni mke mwema ringa naye,
Mke ni mwili wako, ni nani wewe wachukia mwili wako
Nimebarikiwa mnoo...
Hii mingine miwili

1. Parapanda ya Bwana italia siku ile
Atakaporudi Yesu kuchukua kanisa lake
Tujitayarisheni, siku hiyo ya kutisha
Ole kwa wale wote, wasiomuamini Yesu

Ndipo Bwana atasema ondokeni kwangu,
Ninyi nyote mliolaaniwa na Baba yenu,
Wataomboleza na kusaga meno, watakapotupwa kwenye moto wa milele....

2. Unafikiria nini, ulimwengu ni wa shida
Tena unajidanganya wewe, na mambo ya ulimwengu

Kanisani umeacha ulikuwa unategemewa. ...............

Siukumbuki vizuri uuuh

Mpanzi alitoka kwenda panda mbegu njema shambani mwake

Na zingineee, zilianguka njiani
Na zingineee tena, zilianguka kwenye miiba
Na zingine tena, zilianguka pakavu
Na zingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikazaa moja Mia sitini moja thelathini

Kuna mwingine pia, naibia ibia tu.

Hata baada ya siku sita mwokozi Yesu,
Alipanda mlimani na wanafunzi wake........

Sauti iii, Sauti iii
Sauti iii, Sauti ikatoka
Huyu ni mwanangu mpendwa msikilizeni, atakayowafundisha nayashikeni

Sijui wametajwa hawa, Bethel Choir walioimba

Wahurumieni
Mungu yu mwema
Sio sisi
Umepoteza Dira
Basi nasema (tunda la roho) etc
Japo melody na sauti siisikii ila hakika maneno Haya yamenibariki.

Thanks Dada mtumishi HS
 
MUNGU akubariki sana umenikumbusha sana,
Pamoja Mkuu!
kaka kuna wimbo ka jin animeusahau ila nakumbuka baadhi ya mameno yake tu"alipofika karibu aliuona mji akaulilia akisema watu wa yerusalemu"
Nakuangalizia,uwe na subira!
Sauli Sauli mbona waniudhi
Sauli wawatesa watu wangu

Bwana kachukizwa sana, kamwambia Sauli
Mimi ndimi Yesu unayeniudhi
Ole wako wewe, unayemuudhi
Bwana Mungu wako utahukumiwa
Naukumbuka Huo Wimbo,uwe na subira!
Fahari ya vijana, ni ..........
Fahari ya wazee, ni kichwa chenye mvi
Fahari ya moyo wangu, ni kuyatenda mapenzi yake Mungu
Just a sec!
 
Nilinunuaga album zao zote 3 ambazo ziko katika video (ULYANKULU). Nilikuwa nawapenda sana hawa, pamoja na wale akina mama "Wa kwa Mungu hakuna mzee" kutoka Shinyanga ... Hawa wa mama walikuwa wana sauti tamu sana.

Nakumbuka Album hizi na nyimbo zake. Ninazo LAKINI nitawawekea majina ya nyimbo ili iwarahisishie kutafuta.

1. KATIKA VIUMBE VYOTE.
-Katika viumbe vyote
-Palikuwa na mtu (Ayubu)
-Bwana ndiye mchungaji wangu
-Neno la Mungu lililomjia Yona
-Wakati ule wa Nuhu
-Vijana tuamke sote
-Alipofika karibu aliuona mji
-Yesu alipokuwa ameketi.

2. MWENYE MAMLAKA (Mapigano)
-Mwenye mamlaka
-Wakati huo
-Yesu katazama
-Wokovu ni lazima
- Fahari ya vijana
-Safari ya wana wa Israeli
-Ombeni nanyi mtapewa (Paulo & Sila)
-Amri mpya nawapeni (upendo)
-Goliathi
-Kama ndugu yako akikosa
-Sisi ni barua

3. SAMSON & DELILA
-Dunia ya shida
-Samson
-Ufunuo wa Yohana
-Nitamwona Yesu
-Basi nasema
-Yusufu
-Nikifikiria
-Kifo cha Yesu
-Ulimkimbilia Mungu

Kuna hawa nao walikuja juu miaka ya 2000 mwanzoni wanaitwa "THE GOSPEL SOUND SINGERS," kutoka EAGT Singida. Album yao ilibamba sana.

Iliitwa "KILA GOTI LITAPIGWA."
Ilikuwa na nyimbo hizi;
-Wathamani
-Dunia hii
-Kabla sijaokoka
-Yesu tusaidie
-Amechukua masikitiko yetu
-Mwanzo na mwisho
-Mimi najivunia
-Bwana Yesu

Nk...

Dah! Those days!
 
Siku ya kutaabika aaaa siku ya kukanyagwa aaaaa siku ya fujo inakuja itokayo kwa bwanaaaa bwana wa majeshi

Katika Bonde la maono linabomoa kuta na kuililia Milima
Tazamaa bwana anakujaa




Kuna huu mwingine unaimba
Mle kaburini Yesu kazikwa alifunikwa na Giza kubwaaaaa na siku ya tatu bwana kafufuka walinda kaburi waliogopaaaa
Walikiri kwamba Yesu yu hai shangilieni Yesu alifufuka
 
Nilinunuaga album zao zote 3 ambazo ziko katika video (ULYANKULU). Nilikuwa nawapenda sana hawa, pamoja na wale akina mama "Wa kwa Mungu hakuna mzee" kutoka Shinyanga ... Hawa wa mama walikuwa wana sauti tamu sana.

Nakumbuka Album hizi na nyimbo zake. Ninazo LAKINI nitawawekea majina ya nyimbo ili iwarahisishie kutafuta.

1. KATIKA VIUMBE VYOTE.
-Katika viumbe vyote
-Palikuwa na mtu (Ayubu)
-Bwana ndiye mchungaji wangu
-Neno la Mungu lililomjia Yona
-Wakati ule wa Nuhu
-Vijana tuamke sote
-Alipofika karibu aliuona mji
-Yesu alipokuwa ameketi.

2. MWENYE MAMLAKA (Mapigano)
-Mwenye mamlaka
-Wakati huo
-Yesu katazama
-Wokovu ni lazima
- Fahari ya vijana
-Safari ya wana wa Israeli
-Ombeni nanyi mtapewa (Paulo & Sila)
-Amri mpya nawapeni (upendo)
-Goliathi
-Kama ndugu yako akikosa
-Sisi ni barua

3. SAMSON & DELILA
-Dunia ya shida
-Samson
-Ufunuo wa Yohana
-Nitamwona Yesu
-Basi nasema
-Yusufu
-Nikifikiria
-Kifo cha Yesu
-Ulimkimbilia Mungu

Kuna hawa nao walikuja juu miaka ya 2000 mwanzoni wanaitwa "THE GOSPEL SOUND SINGERS," kutoka EAGT Singida. Album yao ilibamba sana.

Iliitwa "KILA GOTI LITAPIGWA."
Ilikuwa na nyimbo hizi;
-Wathamani
-Dunia hii
-Kabla sijaokoka
-Yesu tusaidie
-Amechukua masikito yetu
-Mwanzo na mwisho
-Mimi najivunia
-Bwana Yesu

Nk...

Dah! Those days!
Yesu kawaambia

Na kama ndugu yako akikosa muonye
Akitubu msamehe
Kuliko kumkosesha mmoja wapo,
Wa wadogo hawa
Mkuu,nashukuru!ila waweza tuwekea hizo hapa jf?
 
Back
Top Bottom