Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Kuna wimbo wa Sedekia kuhusu Meshack, Shedrack na Abednego

Je hatukuona watu wanne na huyo wanne ni mfano wa mwana wa miungu?....Mfalme aliuliza...Mfalme aliuliza

Sijui kwa jina unaitwaje huo wimbo.
 
Mkuu kama ilienda shule ya msingi Babati miaka Hiyo kuna uwezo mkubwa tunafahamuana.

Nakumbuka nilikuwa naishi majengo mapya lol.
Mkuu nilisoma shule ya msingi Babati kukiwa na kina mwalimu Lawi, Ufoo,Mashausi Kitundu,Isaka na wengineo kibao...tufatane PM mkuu...nilikuwa nakaa mitaa ya kanisani Lutheran na tulikuwa tunaimba na kujifunza kupiga vyombo na watoto wa mchungaji Mjema
 
Hahhhahahah dahhhh mkuu umenikumbusha mbali.

Nasikia Mwalimu Babu alifariki. Alikuwa mwalimu wangu wa Geography darasa la tatu Lawi alikuwa Mwalimu mkuu na Mwalimu Kitali alikuwa wa hisabati darasa la Tano tulikuwa tunamwita mwalimu Konyeza. Darasa la kwanza na la pili nilikuwa na mwalimu Kawala na Mwalimu Hawa.

Kuna Mwalimu mmoja alihamia kutoka shule ya msingi Maisaka kuja shule ya msingi babati mwalimu Lyamuya sijui kama unamkumbuka alikuwa mkali. Ukimuona tu unakimbia hata kama hukufanya kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…