Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Naomba wimbo wa Kinondoni Menonnite choir wana kunyata uitwao
kazaliwa
 
Hilo ni pambio, kama yale pale kalivari yote yamekwisha.. huwezi pata
Ok. Nimekupata mkuu na ule wa safari ya wana wa israel nahisi uliimbwa na kkkt makongolosi chunya nilishawahi kuisikiliza mika hiyo kwenye zile kanda za zamani lakin kwa karne hii nautafta siupati. Pia katika album hiyo hiyo kuna wimbo unasema " NI NANI ANAEFANANA NA YESU". na pia kuna mwingine wanaimba kwamba ndege wa angani ifika ikifika jioni hurudi kwenye viota vyao. Hebu nisaidie ni album moja hiyo
 
Mapigano ulyankulu (Mwenye mamlaka yote)

Safari yao .

Kuna wimbo wa safsri ya wana wa Israel kabla ya huu na wimbo unapoanza ikishapigwa biti wakianza kuimba tu inaanza hivi
Safaaaari yawana wa israeli
Waliiiipo ondoka kule misri
Wakaianza safari iliyokuwa ngumu wakaivuka bahari, bahari ile ya sham, wakaipita milima, milima ya silai, watembea jangwani kwa muda wa miaka arobaini. Inaimbwa namna hiyo
 
Wadau.. Majukumu yalibana, na mishe za Pasaka.. Nimemalizia mzigo
Mkuu, shukrani sana kwa hizi nyimbo za Kwenye album ya "Unangoja nini".
Kuna track moja (kutoka kwenye albamu hiyo hiyo) ulisahau kuiweka. Inaitwa "Mapambazuko".
Kama unayo, please, tusaidie.
 
Baraka nyingi sana kwa wachangiaji wa huu uzi,mjazwe mpaka zimwagike.
 
Jamani anayeujua ule wimbo unaimbwa something something tuzae matunda kama mbegu ya haradali unaitwaje?
 
 

Wengine wameolewa, wengine waneshahama makanisa nilikuwa hapo Mwaka jana mwezi wa kumi ni sura ngeni na mpya tu ndo niliona kwa hiyo praise
 
hiyo praise ya sas ni wanafunziwa MUCCOBS na KCMC

...nahisi itakuwa hivyo, kipindi kile hadi wanafunzi wa veta walikuwa wanakuja kuabudu pia. Kuna mdada mmoja nambuka alikuwa pale praise mwembamba mweupe anavaa miwani yaan ilikuwa ikifika wiki yake hiyo asubuhi ataimba hadi unaona wachungaji wanafurahi. Mwaka jana sikumkuta niliuliza alipo nikaambiwa ameolewa na amehama kanisa
 
Huu wimbo uliimbwa na kwaya ya kanisa la undugu, wako pale keko/chang'ombe maduka mawili...

Aisee.. ni wa zamani sana... nakumbuka kipindi hicho naabudu pale..

Sikumbuka kama albam yao ilikuwa inaitwaje!!

Mkuu, hebu jitahidi kuniulizia ulizia. Maana ni miaka mingi imepita mara ya mwisho kuusiikiliza huu ilikuwa ni 1999 redioni.
 
Dah, aisee wewe ni hatari sana, Huna namba yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…