Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Nkinga Christian choir Sauli, Sauti ya Jangwani na wimbo wao ningelikuwa na uwezo wa kumlipa mauti daah huu uzi nauwekea lamination kabisa
 
Habarini waungwana
Mwenye nyimbo ya Nitamwandama bwana alienikomboa ule old version hawa ndo naupenda huu uliotoka miaka saba 2013 sijaupenda
.
Na kuna mwimbo wa zamani sijui waliimba choir gan unaimbwa
Yuda alikufa sababu ya kupenda pesa wanadamu wengi tumetawaliwa na pesa pesa inauwaaaaaaaa
Huu wimbo waliimba kwaya fln ya mbeya, nimeshautafuta sana kwa kila njia bila mafanikio. Nimeenda hadi kwa waganga lakini wapiii!!!![emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wakuu mimi natafuta nyimbo za neema grace yule wa arusha aliye imba "nitakushukuru" mwenye albamu yake au nyimbo zake plz aniwekee
Nyingine natafuta nyimbo za dada Joyce alimba mahathi ya taraabu mwenye nazo plz anisaidie maana nimezitafuta sanaa...
 
Kuna album moja ya kwaya ambayo kwenye cassette yake kulikuwa na picha ya kifaru cha vita....nimeisahau jina...kama kuna mtu atakuwa anaikumbuka ile cassette na jina lake atabarikiwa sana

Tumain kwaya Shangilieni St James Arusha - Album inaitwa Nakulia Yehova

 
Kaka, kuna moja ilikuwa inaimba hivi

“Angalieni ndege wale wa angani, hawapandi wala hawavumi. Lakini muumba wetu mwenye uwezo huwalisha kila siku (Mara 2) “
Chorus

“Wale ndege wote wa angani wa angani
Wanakula kwa uwezo wake MUNGU
Kawaumba ndege wake mwenyewe wake mwenyewe
Hawawezi kuwaacha wafe na njaa.”

Hii nyimbo ilikuwa inapigwa sana Radio Tumain mwishoni mwa miaka na 90 na mwanzoni mwa miaka ya elfu 2. Mwaka jana nilijaribu kuwaandikia radio Tumaini kuhusiana na hii nyimbo ila walishindwa kunisaidia huenda wale watangazaji waliokuwepo wameshastaafu au Wapo radio zingine. Sijui unaifahamu & au kuna mtu mwenye ataweza ikumbuka sijui ilikuwa ni choir gani ile[emoji17][emoji1751]
Huu wimbo uliimbwa na kwaya ya kanisa la undugu, wako pale keko/chang'ombe maduka mawili...

Aisee.. ni wa zamani sana... nakumbuka kipindi hicho naabudu pale..

Sikumbuka kama albam yao ilikuwa inaitwaje!!
 
Huu wimbo waliimba kwaya fln ya mbeya, nimeshautafuta sana kwa kila njia bila mafanikio. Nimeenda hadi kwa waganga lakini wapiii!!!![emoji3][emoji3][emoji3]
Nami nimehangaika sana kuupata huu wimbo na nyingine za hii albam yao. Nilikuwa na Cassette yao ila waungwana wakawa wajanja wakajibinafsishia.
 
Daah huu wimbo jamani (japo maneno mengine nimeyasahau)

Mara ngapi nimekukusanya, kama vile vifaranga
Vya kuku chini ya mbawa, lakini umekataaa

Maonyo mengi umesikia, lakini umekataa
Kumbuka usipookolewa, utakwenda Jehanamu
Kuna wimbo sijui iliimba kwaya gani? Haya ni baadhi ya maneno ndani ya wimbo huo "Jerusalem *2 uuae manabii......Msalaba umeku kumbatia kama vile kifanga cha kuku Chini mbawa zake lakini umekataa " Naomba mwinye kujua huu ni wimbo wa kwaya gani anijuze au mwenye wimbo huu anitumie what's app. 0765544791 Natanguliza shukrani
 
Habarini waungwana
Mwenye nyimbo ya Nitamwandama bwana alienikomboa ule old version hawa ndo naupenda huu uliotoka miaka saba 2013 sijaupenda
.
Na kuna mwimbo wa zamani sijui waliimba choir gan unaimbwa
Yuda alikufa sababu ya kupenda pesa wanadamu wengi tumetawaliwa na pesa pesa inauwaaaaaaaa
Pesa inauaaa
Pesa inapotezaa...
 
wakuu naomba mwenye wimbo wa Ambwene Mwasongwe YEYE KATIKA SIKU ZAKE ALIMTOLEA MUNGU IBADA anisaidie nimeutafuta sana bila mafanikio
 
Kuna album moja ya Adona Pentecostal Kibao Cha kwanza linaitwa SITASAHAU HURUMA ZA BWANA alafu Mwisho kabila ameimba sijui kikabila gani SHAKALABE
 
Jamani ubarikiwe sana. Umenikumbusha na huu wimbo pia

1. Kazi yake Bwana Yesu, ya kuokoa wanadamu
Ilikuwa ngumu sana, kwake mwokozi kuimaliza.
(Yesu mwokozi)
Alihuzunika Bwana Yesu moyoni mwake
(Akasema)
Akasema eeh Bwana wangu kikombe hiki
(Kiniepukeeee)
Zipo You Tube....
Amina sana!!
 
Back
Top Bottom