Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Dah, old is gold aiseee.
Kuna ule mmoja una maneno, .....MVUA ILIANZA KUNYESHA BILA KUKATIKAAAAAAA......
Sijui ndo huo wa ktk viumbe vyote??!!!
Alafu kuna ule wa Samson: SAMSONI KWA KUMPENDA DELILAAAAA sijui nini na nini na nini........
Waimbaji ni hao hao mkuu, wanaitwa Barabara ya 13 kama kumbukumbu zangu ziko sawa.
 
Nilipokuwa mtoto nyumbani Casset za Sungura Mjanja zilizorekodiwa Habari Maalum Arusha ndio tulikuwa tunawekewa kila Jumapili....
Hapo ni jioni tumekula, tumeoga tumekaa ndo tunaekewa..

Azarel sungura mjanja haujaangalia..??

Watoto siku hizi wanaangalia CartoonNetwork tuu..
 
Kuna ile hakuna Mungu kama wewe Bwana aanha, anaanha, japo si ya zamani sana ila nafikiri ni ya miaka kama 15 hivi iliyopita si vibaya tukaiweka hapa

Natumia smart phone ya halotel H8501
Fanya hivi:
a)Download Application ya Tubemate,halafu,tumia App hio kutafuta Video Zako Youtube!Uzuri Tubemate Ina Option ya Kudownload Video Kirahisi!
b)Nenda Youtube,Tafuta Halafu Angalia Link ya Hiyo Video!Tumia Opera Mini!
Mara Nyingi Link Zake Huwa Zimeandikwa Ìvi:"https//m.xyz1265.."
sasa fanya hivi, futa ile "m" halafu andika "9x" halafu reload page!
 
Nilipokuwa mtoto nyumbani Casset za Sungura Mjanja zilizorekodiwa Habari Maalum Arusha ndio tulikuwa tunawekewa kila Jumapili....
Hapo ni jioni tumekula, tumeoga tumekaa ndo tunaekewa..

Azarel sungura mjanja haujaangalia..??

Watoto siku hizi wanaangalia CartoonNetwork tuu..
Nimeangalia sana nikiwa mdogo

Halafu kulikuwa na lile gari la "SINEMA LEO" la Arusha walikuwa wanatuletea nayo hizi filamu shuleni.
 
Kuna kwaya moja hivi ilishika sana ilikuwa ikiitwa kamenyula kama ntakuwa sijakosea spelling.

Naweza kupata album yao?
 
Fanya hivi:
a)Download Application ya Tubemate,halafu,tumia App hio kutafuta Video Zako Youtube!Uzuri Tubemate Ina Option ya Kudownload Video Kirahisi!
b)Nenda Youtube,Tafuta Halafu Angalia Link ya Hiyo Video!Tumia Opera Mini!
Mara Nyingi Link Zake Huwa Zimeandikwa Ìvi:"https//m.xyz1265.."
sasa fanya hivi, futa ile "m" halafu andika "9x" halafu reload page!
Na ku-upload nyimbo hapa inakuwaje maana nimetafuta sijaona kila nikiweka kwa kutumia attachment option inakuwa ipo faint na nafikiri ni kwa ajili ya docs.
 
Haya ndio mambo sasa!!
Unaburudika na kupata ujumbe barabara.

Ujumbe unaokufanya utafakari neno la Mungu.
Ubarikiwe mleta mada.
Umeuliza kuhusu Sedekia na RHM, ni kwamba Sedekia alishaimba na New Life Band, kama unawajua hawa vijana na band yao.

Ila Tanzania nzima walikuwa wanarekodi RHM.

Sidhani kama itatokea tena Gospel band kama NLB Tanzania

Na sio Sedekia tu ila pia kuna Upendo Kilahiro na Beatrice Muhone.

NLB Walitunga mapambio kama:-

- Iende mbelee injili hiyoo...iende mbeleee

- Ainuliwe Mungu wetu leooo...ainuliwe bwana wa mabwana

- Mji ulee una meremeta umepambwa mauaaa

Unakumbuka?

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom