Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Nashukuru sana brother nimebarikiwa kwakweli
Ahsante mkuu
Hizi nyimbo zina nikumbushaga mbali sana
Kipindi nyimbo za gospo zilikiwa gospo kweli, na ndio maana zinadumu mioyoni mwa watu miaka na miaka
 
Kweli kabisa zilikua zina ujumbe mzito kuliko vinanda na magitaa...nyimbo za siku hiz magitaa na vinanda vimemeza ujumbe
Aaah
Sasa mheshimiwa DC, waimbaji wenyewe kama ndio hao hao ma producer wa ben pol, mara wawatungie nyimbo watu wa bongofleva, hahaha
Ki ujumla lazima tutasikilza za zamani tuu hakuna namna
 
Jamani mi ombi langu mwenye Album ya Victoria singers television ya maisha nyimbo zilizokuwemo ni pamoja na wapendwa watu wake mwokozi, amezaliwa, yerusalemu n.k.
Pia hao hao victory singers lile tunda la roho. Yaani kifupi kwaya ya kinondoni Victoria singers ile ya zamani sio hii ya mtu wa nne
 
Nielekezeni jinsi ya kuiapload nyimbo humu hizo za zamani ninazo Ila sijui zinawekwaje humu
Tumia Web browser mkuu kama Google Chrome, Firefox au opera mini. Jamii app haikubali kufanya upload ya audio, videos.
 
Ingawa mimi sio muumini wa kikristo, lakini wimbo huu unaendana na maagizo ya dini ni nayo iamini, ndio maana ninaupenda
Huo wimbo unakumbusha wanadamu wote kuwa kuna "kufa" na kuna "Hukumu" na kila mtu atasimama peke yake siku hiyo.
 
Jamani kuna kwaya siikumbuki jina ila nakumbuka mistari ya nyimbo zao mbili tu, kama kuna member anazijua au anazo atakua amenipa zawadi kubwa kuliko zote mwaka huu 2016.

[1] Bwana mungu amekuumba mweusi Mungu amependezwa na weusi wako.

Bwana mungu amekuumba mweupe Mungu amependezwa na weupe wako.

Ajabu kwamba watu hawathamini uumbaji wake Bwana Mungu baba,

Wamesahau kwamba wao mavumbi na huko tutarudi kwake Bwana.

Wimbo wa pili nakumbuka mistari michache tu,

Nikupe nini Mungu wangu eeh mungu wangu, ulinipa bila kuomba mimi eeh Mungu wangu. Kila kitu ni mali yako baba eeeh Mungu wangu.

Shukrani in advance watu wa Bwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…